✍️ SEMINAR ✍️ TOPIC; MAOMBI ✍️VETA DAKAWA 2020

SEMINAR :TOPIC: ✍️👊 MAOMBI

Mwalimu; Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768

Tufunue Vitabu hivi;2Mambo ya nyakati:7:14-16 1Wafalme;8;38-49 Zaburi;61;1,86;6 1Petro;3;12

SOMO HILI AU WALAKA HUU UNASURA "5"

A:MAANA YA MAOMBI

B; MAKUNDI YA MAOMBI

C;SEHEMU ZA MAOMBI

D:TABIA YA MAOMBI

E: HITIMISHO


                     UTANGULIZI.

👊✍️SIKU YA KWANZA; Tarehe 3/8/2020 Jumatatu muda saa;4;00-6;00

A👊👊MAANA YA MAOMBI NA UFAFANUZIq WAMAOMBI 👊👊

1:MAOMBI NI NINI??Ni Hali ya uwasilishaji wa Taarifa na maendeleo ya Mtu Kiroho na Kimwili mbele Za Mungu Yenye Kutaka Apewe Majibu na Anachokiomba Nakukiamini.

B👊👊✍️KUNA MAKUNDI MAWILI YA MAOMBI;(WANAPOOMBA)

✍️Kundi la Kwanza Ni la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua
✍️Kundi la Pili Ni la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua

C:KUNA SEHEHEMU TANO ZA MAOMBI MTU ANAPASWA AZIJUE.

1:AINA ZA MAOMBI ANAZOPASWA MKRISTO AOMBE

2;MIKAO YA MAOMBI ANAZOPASWA MKRISTO AKAE WAKATI ANAOMBA

3;STAYLE ZA MAOMBI MKRISTO ANAZOPASWA APITIE

4:MBINU ZA MAOMBI NAKUKABILI TATIZO MKRISTO ANAVYOPASWA

5;MUDA WA MAOMBI MKRISTO ANAOPASWA AOMBE

D:TABIA YA MAOMBI
✍️Tabia ya Maombi ya Mazoea
✍️Tabia ya Maombi ya Kujitoa
✍️Tabia ya Maombi ya Nguvu
✍️Tabia ya Maombi Madhaifu yasiyo na nguvu.

E; HITIMISHO
Hapa Somo Letu Na Semina Ya Wiki moja Kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili Itakuwa imeisha

KARIBU Semina YETU
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

SEHEMU: A : MAANA YA MAOMBI

Maana Sahihi ya Maombi Ni Pumzi Yenye uhai wa mkristo yoyote yule ili ukristo wake uimarike Unaitajika Maombi "AFANYE MAOMBI"

MAANA HALISI MAOMBI 👊✍️Ni uhai wa mtu aliyeokoka au mwokovu a

Maana ya Pili; Maombi Ni Uwasilishaji wa maendeleo ya Mtu mbele za Mungu Yenye kutaka Apewe jibu juu ya alichokiwakilisha.

NANI ANAPASWA AOMBE ?
Ni Mtu Yeyote Yule ANAPASWA aombe Juu ya anachokitaka kwa Mungu


KATIKA UWASILISHAJI MTU  MAOMBI HUWA YANAWEZA

1;Kuchukua Muda Mrefu 

2;Kuchukua Muda Mfupi


MAOMBI YA KUCHUKUA MUDA MREFU NI MAOMBI Yanayochukua muda mrefu mtu mpaka Apokee inaweza kuchukua mwaka Kuchukua Miaka mtu ndio anajibiwa

MAOMBI YA KUCHUKUA MUDA MFUPI hii huwa ni Maombi Yenye kuchukua muda mfupi mtu anapokea hitaji lake.

2mambo ya nyakati : Mlango 7


15 Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa



TUNÀENDELEA SURA YA PILI; ✍️SEMINAR SIKU YA PILI✍️Jumanne;4/8/2020

Muda Kuanzia Saa;4;00-6;00


Tumeshaona Maana ya MAOMBI Katika Sura "A" Jana Tumejifunza Maana HALISI ya MKRISTO MAOMBI YANAMAANA GANI??


Maswali Ya Jana Yalikuwa??:

Kwanini Tunaomba hatujibiwi Wakati Baba Yetu Anatuombea Mbinguni "Yesu Kristo""?

Jibu;

Baba Yetu Alituagiza nasisi tuombe tusikae na kusema Yupo Yesu Ananiombea Wakati wewe umekaa Akasema amfatae lazima ajitaambishe kuutafuta Ufalme  wa Mungu

Luka : Mlango 11:9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa


KARIBUNI Tuendelee,,,,,,

SEHEMU B; MAKUNDI YA MAOMBI 

Jumanne@4/8/2020
Morogoro Veta Dakawa
Mwalimu Pastor Richard

KUNA MAKUNDI MAWILI YA MAOMBI

1:Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua

2;Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua


Tuanze Kujifunza Kuangalia Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wanaemjua

Hili Kundi likoje Tutaliona nakujifunza mengi.


1;KUNDI LA WATU WANAOMUOMBA MUNGU WANAEMJUA.Yohana:14;25-26

Hili Huwa Ni mkusanyiko wa wakristo waliopata Neema ya Kumjua Mungu wao Vyema Kupitia Neno la Mungu kuona Kujifunza.


Maana ya Pili ni Watu wanaojua vyema UWEZO wa Wanachokiamini Nakukitumaini.


MUNGU NI NANI?

Mungu Ni roho aliyeziumba roho zingine hii ukijua Ni rahisi Kuelewa kipi unapaswa Ukiombe.


CHOCHOTE KILICHOUMBWA NA HII ROHO; Hupaswi kukiomba au kuaminishwa Ukiombe katika maisha yako ya ukristo Ujue Mungu wako Ni ROHO.

Mfano Wapo watu huomba Mizimu na Wegine Wapo ndani ya kanisa Wegine Ni Manabii Wachungaji au Wanamaombi Wazuri Kumbe roho za mizimu zinawapa mafunuo na kuwaelekeza wakatoe Sadaka wengine wakaabudu Makaburini Usiku wa manane

Wapo watu huamini majini mazuri na huwa Wanaanza kuyaomba mtu Yeyote Yule atakayeabudu au Kukiomba Kitu KILICHOUMBWA na Mungu huwa Tunasema Anaabudu au Kumuomba Mungu asiyemjua Tukisimama na Kumwabudu na Kumuomba Mungu wa Kweli Mungu hujibu tusimchanganye tu


MUNGU WA KWELI NI MSAFI HAPENDI UOVU.

Ukiingia Kwenye Maombi uingie ukiwa hauna uchafu hujamuweka mtu maana  Mungu wako Ni Msafi ukiingia Kuomba TU ukaomba huku umemuweka mtu au huachi pombe huachi Uchawi huachi Uzinifu huachi kutokuwasamehe watu ujue Utakuwa umejiondoa katika Kundi la Watu wanaomjua Mungu.

IMANI YENYE KUMJUA UWEZO WA UNAEMUOMBA

Kabla ujaomba lazima akili yako ijipime Mungu uliye nae Anaweza Yote Au Mengine Ni Wewe unaweza Kuyatatua

UJue Kwamba Mungu hujishughulisha Sana NA YALIYOKUSHINDA KWA AKILI YAKO NA UFAHAMU WAKO

Mambo yanayotatulika kwa Akili na Ufahamu wako huwa Anaachia Akili Yako na mastiff yako ifanye kazi.


Wapo watu Wanamchanganya Mungu Sehemu wanapopaswa watumie akili wao wanatumia nguvu sehemu wanapopaswa watumie Ufahamu wait wanatumia Pesa au Maombi


MUNGU WA KWELI ANATHAMINI SANA AKILI NA UFAHAMU

Kwa hiyo sio kila Kitu uombe vitu vingine vinaitaji utumie akili tu na Ufahamu

MAMBO YANAYOMDHIHIRISHA MTU ANAE OMBA MUNGU WANAEMUJUA

1:Huwa wanakuwa Waaminifu Kati yao na Mungu

2;Huwa Wanatumia Akili na Ufahamu pale pakutumia Ufahamu

3:Huwa Na nguvu ya Kumtengemea Mungu

4: Huwa Wanaamini Ubatizo Ufufuo na Ukombozi wa nafsi 

5:Huwa Wanaamini Sio Kila anenae kwa Roho Ni Roho Mtakatifu

6;Huwa wanamaandalizi ya Maombi

7;Huwa wanajitenga Mbali palipo na uwepo wanapoomba

8:Huwa wanajua vyumba Vya Maombi

9;Huwa wanajua Tabia za Maombi

10;Wanajua umhimu na Maana Ya Maombi

Hizi Ndio Dalili Zinazomjulisha Mtu aombaye Maombi kwa Mungu Anayemjua


2:KUNDI LA MAOMBI YA WATU WANAOMUOMBA MUNGU WASIYEMJUA

Hili huwa Ni Kundi la Watu Wanaomuomba Mungu Wasiyemjua nakutambua uwezo wake 

Hawa Ni wapinga Kristo na Wapaganii au Muumini Anayeabudu KILICHOUMBWA na Mungu huyo naye Huhesabiwa Anaenda tu kanisani kukiabudu asichokijua 


MUNGU ASIYEJULIKANA NI

1:Mizimu

2:Mapepo ya uaguzi kusoma nyota nk

3:Majini Kuyaabudu nakusujudia

4;Wachawi na Waganga huabudu Mungu Asiyemjua.


Tabia za Mungu Asiyemjua

1;Kukuongoza katika Uharibifu wa maisha yako au Wegine

2;Ulevi,Uzinzi,na Uchafu wote anakuogoza nakanisani unaenda unasimama Madhabahuni

3;Hukutazamisha Imani ione Pito linanguvu kuliko Mungu.


MAMBO YANAYOMDHIHIRISHA MTU ANAE OMBA MUNGU WASIYE MJUA

1;Huwa Mioyo Yao inaingia Maombi wakiwa nakinyongo

,2;Huwa Wapo gizani Wegine Hawajui Kama Wapo na Mungu wasiomjua

3:Huezi Mira na Matambiko ya kwao 

4;Hurishana vitu na kutumikia miungu migeni

5:Huwa hawajui Uwezo na UKuu wa Mungu wa Kweli

6:Wanatumika na Ushirikina Uganga hirizi na mafundo.

7:Huwa Wanaamini waganga Ndio Tiba kwao

8;Huwa Hawapendi Maombi

9;Huwa Hawataki Habari za Wokovu wa Mungu

10;Huwa Hawajui Maana na uhalisia wa Maombi kwa mkristo


Hizi Ndio Dalili Zinazomjulisha Mtu aombaye Maombi kwa Mungu Asiyemjua.


Kesho Tutaendeleaa Sura ya 3; SEHEHEMU KUU 5 ZA MAOMBI


SWALI;

Kwanini watu Wasiomjua Mungu Wanamuomba Mungu  na Anawajibu Kwanini Sisi tunamuomba Mungu na hatujibu..?

JIBU;Watu wasiokuwa wa Mungu wasiomjua Mungu humuomba mungu sio Mungu 

Kwa hiyo huwakilisha utawala wa Shetani Ambao Upo unamiliki 

1Wafalme;18:35-40

2mambo ya nyakati : Mlango 33

18 Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli


LEO NI SIKU YA TATU YA SEMINA YETU JUMATANO LEO TUPO SURA YA 3

TUNÀENDELEA a....

Tumeshaona Maana ya MAOMBI na Makundi ya Watu Wanaomba Leo Tunaangazia Sehemu Tano au Vyumba vitano vyakuingia unapoomba TUTAINGIA CHUMBA KIMOJA KIMOJA ILI UELEWE

🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🖕🍒🍒🍒🖕🍒🍓🍓🍓🍓

"Sura ya 3; SEHEMU KUU TANO ZA MAOMBI"

TUTAINGIA CHUMBA KIMOJA KIMOJA KATIKA CHUMBA 

CHUMBA CHA KWANZA; Karibu Tuingie Tukione 

Seminar Jumatano Tar;5/8/2020

Mwal Pastor Richard 

Mwadaaji:Roho Mtakatifu

💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪

CHUMBA CHA KWANZA "✍️AINA ZA MAOMBI ya  MAOMBI MKRISTO ANAZOPASWA AOMBE.

Mkristo Unapaswa Ujue Aina Za Maombi Unazopaswa Uombe Na Hii itakusaindia Kupambana Vyema Kiroho Sio Kwenda kwenda TU au Kuomba Omba tu.

Kuna Aina Tano za Maombi Mkristo Unapaswa Uzijue

1:Maombi ya Sifa na Toba

2:Maombi ya shukrani

3:Maombi ya Vita na Ukombozi

4:Maombi ya wote 

5;Maombi ya Binafsi peke yako


1:MAOMBI YA SIFA NA TOBA

Haya huwa Ni Maombi unayopaswa umsifu Mungu nakumtukuza kwa Yale machahe anayokutendea Na Utubu pale ulipowaza au Kufikiri kinyume kwa Ajili yake

✍️✍️MAOMBI YA SIFA✍️✍️

Zaburi : Mlango 143

7 Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea;Usinifiche uso wako,Nisifanane nao washukao shimoni

MAOMBI YA SIFA YANAKUWA HIVI

:1 Tamka umwinue Mungu na Umsifie ✍️mfano;Hakika wewe Bwana unaweza hata Hili nililofikilia Kuwa ngumu Kwako KUMBE ndogo Sana Haleluyaaa Bwana Unanifurahisha Nasema Shetani na ugonjwa huu kwangu hauniwezi maana ninae Baba mwenye nguvu Katika jina la Yesu Amen 🙏

2; Sifu Matendo Yake hata Kama unamuona Kachelewa✍️Mfano:;Nikakupigia Makofi Bwana wa Mabwana Ansate kwa Kujibu nilichokuomba Unajua Baba Nakupenda Sana sababu kila nikiomba unajibu Na sema pokea Sifa halafu piga Makofi kwa Bwana.

3;Cheza Sifa Kabisa✍️Mfano: Imba Mimi Ni Wa Juu..Juu Juu Sana Shetani Ni was chini...chini Sana

Wimbo 2;I Love you Dady...I Love you Dady  Forever I Love you Dady..

Sifu huku Ukicheza.

4;Abudu Kwa Moyo Wote✍️Mfano;Amen,,Amen,,Amen,, Haleluyaaa Haleluyaaa Ha..le..luyaaaa


TOBA

Unatakiwa Umuombe MSAMAHA Mungu kila unapomkosea

Mfano;Piga Magoti uombe Eeh Bwana Naomba unisamehe nimekuwa nikinug.unika nikiwaza mabaya nisamehe Baba yangu 🙏🙏


2;MAOMBI YA SHUKURANI

Haya huwa Ni Maombi unayopaswa uombe Umshukuru Mungu Kila wakati kwa wema wake.

 2Wakoritho : Mlango 9

11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu

MAOMBI YA SHUKURANI YANAKUAJE

1;Tamka Maneno ya Ansate nyigi ✍️Mfano;Ansate Bwana,,,Ansate Yesu Umefanya kwangu,,,Nakushukuru Wewe Bwana

2:Thamini Madogo Madogo Unayotendewa✍️Mfano; Hili Mimi Namshukuru Mungu Tu

3;Kumbuka Aliko Kutoa Mungu✍️Mfano;Yaani Mimi Nilikuwa nife lakini Mungu aliniokoaa

44

3;MAOMBI YA VITA

Haya huwa Ni Maombi ya kupigana nakunyaganyana Umiliki wa Kitu kwa nguvu ya Kiroho hii huwa Unatakiwa Upambane Kiroho Vita Kweli Kweli.

 2Wakoritho : Mlango 10

3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili

MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA MAOMBI YA VITA.

1:Usiweke mtu moyoni au Mawazo✍️ Mfano:Unaomba huku Unamtu umekosana nae utapingwa tu.

2;Tamka Maneno kwa Kukaza Ulimi au Amri✍️Mfano;Achia Toka Pingwa

3:Kuwa Makini Unapotaja YESU usitaje yesu Neno la Mungu tumia vizuri.

Neno linasema hatupingani Kimwili Nakupinga Pingaa Kwa Jina La Yesu 2wakoriho:10:5 Kila Elimu iliyojiinua mbele yangu naivunja nabomoa kwa Jina La Yesu...endeeleeeeaaa

4:Tumia Siraha hizi

MOTO WA YESU

Mapanga

Roho Mtakatifu

Malaika wa Vita/Moto

Jina la Yesu

Neno

Na Siraha za Kimwili zilete katika Roho..

5:Omba huku Unatembea na Kufanya Kitendo

6;Kabla hujaanza Omba Malaika wa Maombi ya Vita

7:Ukimaliza Yafunike Kwa Damu ya Yesu Maombi Yako


4;MAOMBI YA WOTE

Haya huwa Maombi yanayoombwa na wote watu zaidi ya mmoja

MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA HAYA MAOMBI

1:Tamka kuwaombea wengine✍️Ombea wagonjwa Wenye HITAJI

2;Ombea watu Wengine eidha kwa Makundi Makundi au Kwa Majina✍️ Mfano Naombea Wagonjwa Katika jina la Yesu 🙏 Naombea wadongo Zangu wafaulu mitihani Yao....

3;Wafunike Kwa Ulizi wa Mungu.


5: MAOMBI YA BINAFSI

Haya huwa Ni Maombi yakujiombea mwenyewe TU usiombee Wegine.

MAMBO YA KUFANYA UNAPOOMBA

1;Tamka maneno yakujiombea mwenyewe TU✍️Mfano;Mungu Unisaidie nipate kazi

2;Kumbuka kuyafunika kwa ulizi Maombi yako.


CHUMBA KIMOJA TUMEKIMALIZA KESHO Tutaendeleaa Chumba Cha Pili Cha Maombi

✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️✍️💪🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕🖕

KARIBUNI KATIKA SEMINAR SIKU YA 4 ALHAMIS

Tar:6/8/2020

Mwal; Pastor Richard

  CHUMBA CHA 2:MIKAO YA MAOMBI 

MIKAO MAANA YAKE✍️Ubunifu wa Kuomba Kama mkristo UNAJUA UBUNIFU WA KUOMBA

KUNA MIKAO 6 YAKUOMBA

1;MKAO WA KUSIMAMA

2:MKAO WA KUPIGA MAGOTI

3;MKAO WA KUSUJUDU

4;MKAO WA UMEKAA

5;MKAO WA UMELALA

6;MIKAO WA KUTEMBEA


MOJA; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UMESIMAMA

Imeandikwa; "Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”(LUKA  18:10-14)


“Akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akainyosha mikono; (maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni); akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote; uliyemtimizia mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidi; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.” (2 NYAKATI. 6:12-15).

MAOMBI YA KUSIMAMA YAOMBE WAKATI GANI
1;Ukiwa Upo katika mapambano ya Kiroho
2;Katika Vita ya Kiroho
3;Wakati Ukiwa hujachoka Mwili wako 
4:Mwenye Afya na mzima wa viungo


JINSI YAKUOMBA
1;Tamka maneno yasikike
2:Lenga Shabaha yako
3;Piga Makofi au Mwili wako Utikisike 
4:Utaomba Kwa Kawaida 

MBILI; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UMEPIGA MAGOTI

Sulemani alimwomba Mungu akiwa amepiga magoti, “Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yoteĺ, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, HAPO ALIPOKUWA AMEPIGA MAGOTI, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.” (1 FAL. 8:54)



Ezra aliomba akiwa amepiga magoti, “Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu; nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni.” (EZR. 9:5-6)

Danieli aliomba akiwa amepiga magoti, “Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu ;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.” (DAN 6:10)

Mtume Paulo pia alikuwa na kawaida ya kuomba kwa kupiga magoti, hizi ni baadhi ya aya zinazothibitisha hilo, “Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu, wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.”(MDO 20:36) soma pia EFE. 3:1, MDO 9:40

“Hata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba; na baada ya kuagana tukapanda merikebuni, nao wakarudi kwao.”(MDO. 21:5-6). Yesu pia wakati mwingine aliomba huku akiwa amepiga magoti, LUK. 22:41-43)

MAOMBI YA KUPIGA MAGOTI
1:Piga Magoti Kisha kusanya mikono au nyosha Juu
2;Omba Kwa Kuungua na Unyenyekevu
3:Omba wakati unamuitaji Mungu Ajibu



TATU; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UMESUJUDU

Iko mifano mingi ya watu waliokuwa wakiomba huku wamesujudu, Musa, Yoshua, Haruni na watumishi wengi wa agano la kale waliabudu na kufanya maombi huku wakiwa wamesujudu. Yesu Kristo aliomba huku akiwa amesujudu.  “Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana, saa hiyo imwepuke. Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.” (MARK. 14:35).

“Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. Na Walawi, wa wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.” (2 NYAK. 20:18-19)


“Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama; Ezra akamhimidi Bwana, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu Bwana kifudifudi.” (EZRA. 8:5-6)


MAOMBI YA KUSUJUDU
1:Utasujudu chini
2:Utaomba Kwa Kuugua
3;Utanyenyekea 
4:Utaeleza haja nakuuliza maswali

NNE; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UMEKAA

Tunapoichunguza Biblia tunagundua kuwa mtu anaweza kuomba akiwa amekaa, Kwa mfano, mfalme Daudi ni miongoni watu ambao Biblia imewaonesha alimwomba Mungu akiwa amekaa kwenye kiti, Imeandikwa; “Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za Bwana, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.” (2 SAM. 7:18-19)

MAOMBI YA KUKAA
1:Utaomba ukiwa Safarini
2Utaomba ukiwa huwezi kuinuka
3:Utaomba Maombi ya kawaida tu

TANO; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UMELALA

Ipo pia mifano katika Biblia ya watu ambao walimwomba Mungu usiku wakiwa katika vitanda vyao. Wakiwa wamelala vitandani mwao wakamkumbuka Bwana na Kumuomba. Mfano mwingine ni mfalme Hezekia alimwomba Mungu akiwa amelala kitandani kwake na Mungu alimsikia, Imeandikwa; “Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana, akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.” (ISA. 38:1-5)


“Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku. Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.”(ZAB. 63:6-7). Wakati mwingine watu walisujudu katika vitanda vyao na kumwomba Mungu, "Na tena, watumishi wa mfalme walifika, ili wambariki bwana wetu mfalme Daudi, wakisema, Mungu wako na alikuze jina la Sulemani kuliko jina lako, na kukifanya kiti chake cha enzi kuwa kitukufu kuliko kiti chako. Naye mfalme akainama chini juu ya kitanda chake. Na tena, mfalme akasema hivi, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenipa leo hivi mtu wa kuketi katika kiti changu cha enzi, nayo macho yangu yakiwa yanaona hayo. (1 FAL. 1:47).


MAOMBI YA KULALA
1:Utaomba ukiwa mgonjwa
2:Utaomba wakati Ukiwa hujiwezi 
3:Utaomba Usiku ukiwa unalala
4:Maombi ya kawaida sio ya Vita

SITA; UNAWEZA KUOMBA HUKU UKIWA UNATEMBEA

“Elisha alipofika, akaingia peke yake chumbani na kuona maiti ya kijana kitandani. Basi, akafunga mlango na kumwomba Mwenyezi-Mungu. Ndipo akajilaza juu ya mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, na macho yake juu ya macho ya mtoto na mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Na alipokuwa amekaa hivyo, mwili ukaanza kupata joto. Elisha akatembeatembea chumbani, kisha akarudi na kujilaza tena juu ya mtoto. Mtoto akapiga chafya mara saba, halafu akafungua macho.” (2 FAL. 4:32-35, BHN)


Kwa ujumla Biblia halijamlazimisha mtu aombe kwa mtindo fulani, ila sisi wanadamu ndio tumeweka taratibu fulani fulani na kuzifuata kama miongozo katika madhehebu yetu. Ni muhimu sana ukampa uhuru Roho Mtakatifu akuongoze uombeje na usifungwe na taratibu au mazoea ya kidhehebu, kwa maneno mengine unaweza kuomba kwa mtindo wowote ule ili mradi tu usipingane na neno la Mungu.

MAOMBI YA KUTEMBEA
1:Omba wakati Ukiwa Vitani
2;Omba katika Kipindi Kigumu
3:Omba  unatembea tembea
4:Omba Ukiwa Hujajichokea 
5:Huwa Ni Maombi ya mapambano



MIKAO YA MAOMBI INAKUSAINDIA WEWE UNAPOOMBA
1:Usichoke Haraka
2:Ukabiliane na Adui bila Kuchoka
3;Ujue Utayari Wakati Sahihi ya Kupambana
4:Uombe Kwa Ubunifu na Ufundi
5:Utamke kwa Ubunifu
6;Ushinde Vita Kwa Ubunifu tu.


SWALI: Mkao upi huwa unautumia na Unakuwa na nguvu ya Kuomba ??

JIBU;Mkao wa Kutembea na Kupiga magoti.


TUMEISHIA HAPA CHUMBA CHA PILI KATIKA SEHEMU KUU TANO ZA MAOMBI TOPIC✍️ MAOMBI

KESHO Tutaendeleaa Chumba Cha Tatu "STAYLE YA KUOMBA" muda saa:4:00-6:00


KARIBUNI KATIKA SEHEMU TANO ZA MAOMBI LEO TUNAJIFUZA STAYLE YA MAOMBI

CHUMBA CHA TATU; STAYLE YA MAOMBI SEMINA SIKU TAR.9/8/2020 

MKRISTO UNAPASWA UJUE STAYLE ZINAZO SABABISHA UOMBE MAOMBI YENYE NGUVU

Kuna STAYLE ,5 Za Maombi

1:STAYLE YA KWANZA WEWE KUMJUA MUNGU NA UWEZA WAKE
Uweza wa Mungu Ni Hali ya Mtu kujua na Kuwa naufahamu wa juu kuchunguza ukuu wa Mungu nakisha Kumuomba.

Mfano Sahihi.
Ukiwa umesomea Kitu Utaomba kazi Kupitia Elimu uliyoisomea kwa Kuwa unakijua.

Kwa Mungu tunamuomba Mungu Jambo tukiwa tunajua Anaweza.

2:STAYLE YA MAOMBI ENDELEVU HII HUWA YA KUMBA BILA KUKATA TAMAA.
Mkristo Anapaswa awe na Maombi yasiyoisha unaomba bila Kuchoka

3:STAYLE YA MAOMBI YA IMANi
Unatakiwa Imani Yako uone umejibiwa hitaji lako

4:STAYLE YA KUSIFU NA KUCHEZA
Cheza tu na mwimbie Mungu to 

5:STAYLE YA UTOAJI KWA MUNGU
Maombi haya hulengwa mtolee Bwana Pesa 

6:STAYLE YA KUSHIRIKISHA.
Maombi haya hukuhusu Mshirikishe mwingine

,7:STAYLE YA MAFUNDISHO YA NENO.
Maombi yanayohusu Tu Masomo mbalimbali unaponywa

8:STAYLE YA USHUHUDA
Maombi haya hulenga Ushuhuda TU uongee Habari za Shuhuda

9:STAYLE YA KUSOMA BIBLIA 
Maombi haya hulenga usome tu Biblia utafakari Neno

10:STAYLE YA UKIMYA MKUBWA
STAYLE hii itakupasa ukae sehemu pa ukimya Tulia tu.

Naishia Hapa STAYLE ZA MAOMBI TUKIJA KESHO TUTAONA MBINU ZA KUOMBA 



TUNAENDELEA NA SEMINA YETU YA MAOMBI LEO TAREHE;10/8/2020  JUMATATU 

Tumeshaona Maana ya Maombi Makundi ya Maombi Sasa Tupo Sehemu Kuu Tano za Kuomba Wewe Kama Mkristo Uzijue Kama ulipitwa Soma hapa Donoa ingia✍️✍️✍️
✍️ SEMINAR ✍️  https://mchungajirichardi.blogspot.com/2020/08/seminar-topic-maombi-veta-dakawa-2020.html✍️ 
📯
LEO TUNAINGIA KUONA (D)MBINU ZA KUOMBA KAMA MKRISTO.

KUNA MBINU KUU TATU ZA KUOMBA KAMA WEWE MKRISTO.

1:MBINU YA KIJESHI.
2;MBINU YA KIFALME.
3:MBINU YA KIKUHANI.

1:MBINU YA KIJESHI  (1.Samweli.17)
Hii huwa mbinu inayomtaka Mkristo kukifata Kitu katika roho na Kukishambulia kwa Siraha za Kiroho Kwa Lengo lakuteka hicho Kitu na Kukimiliki na Kukitawala katika Roho na Kudhihirika Katika mwili.


MAOMBI HAYA Huwa Ni mkusanyiko wa Maombi ya Vita Yote hutakiwa utumie mbinu za KIJESHI Katika ulimwengu was roho.

Mfano: OMBA HIVI;- Mimi Richard kuazia Leo nateka nakushika Uchumi wa Morogoro Tanzania Africa na Duniani Kila Anga lilozuia Naliangusha nakukipinduwa Katika utawala wake Nawatala Mimi Uchumi ninauvuta Kama Sumaku kwa Jina la Yesu mnazaret🙏🙏
OMBA DAKIKA 10 Ukirudia rudia kaza SAUTI



2:MBINU ZA KIFALME (Esther. 5)
Haya huwa Maombi ya Umiliki na Utawala Katika Ulimwengu wa roho na mwili humtaka mtu awe mkali na mwenye mamlaka Yenye nguvu ya Kuvitiisha Vitu Vinatii na Kusikia Alivyotamka.

MAOMBI HAYA 
Usiwe na Hofu
Umjue Mungu wako
Uwe na SAUTI Yenye Amri

Mfano utakavyoomba

Namiliki na Kutawala Afya Uchumi Ardhi maana Neno la Mungu linasema Mimi Richard Nitaingia Popote nitakapopakanyaga tu nitakuwa nimetawala Na Sasa Natawala Kata ya mbigiri wilaya ya kilosa mkoa wa Morogoro Nchi ya Tanzania na mabara Yote Yoshua;1;3 Ikadhibitike katika ulimwengu wa roho kwa Jina la Yesu.🙏🙏

3: MAOMBI YA KIKUHANI:( 1wafalme.18.)
Haya huwa Ni Maombi Ya Utambulisho na Udhihirisho Kuzimu na Shetani Akujue Katika Ulimwengu wa roho na watu kukujua wewe Ni Nani kuheshimika Kumilikishwa Kuletewa Baraka mbalimbali na watu mbalimbali.

MAOMBI HAYA
Hukutaka uwe umeshaudhibiti kwanza ulimwengu wa roho unaweza kujisimamia mwenyewe na Unamuona Mungu Kupitia Yale unayoomba

Huwa unapaswa Ujitambulishe ulimwengu wa roho ukujue Shetani akikujua wewe Ni Nani utaweza kuupinga Ufalme wa ngiza utaweza kuusimamisha Ufalme wa Mungu.


E:MUDA WA MAOMBI
Muda wa Maombi mazuri Alfajiri saa:11-12Asubuhi

Saa Saba mchana mpaka Saa Kumi.

Usiku Omba saa nane Usiku mpaka Alfajiri

Muda huu Ufalme wa ngiza hushambulia Wanamaombi wasiombe ili wazidi Kuliangusha KANISA na watoto wa Mungu.

Kesho Tutaendeleaa Tabia Za Maombi Endelea Kujifunza Mengi Tumemaliza Sehemu Kuu Tano za Maombi

KARIBUNI MWENDELEZO WA SEMINA LEO TUNAJIFU TABIA ZA MAOMBI TAREHE 11/8/2020


TABIA ZA MAOMBI 🖕👉Taratibu za Uombaji na Maombi Menyewe

MAOMBI YANATABIA MOJA TU Hubadilika nakuleta matokeo ya muombaji Anavyoomba


KUNA TABIA 4 ZA MAOMBI
1:Tabia Yenye Mazoea
2:Tabia Yenye Nguvu
3:Tabia Yenye Uzaifu
4:Tabia Yenye Kujitoa

1;TABIA YENYE MAZOEA
Haya huwa Ni Maombi ya Mazoea Yanayoombwa na watu kimazoea tu.

MFANO
Umeingia Kanisani au Maombi Simu iko wazi unapigiwa 
Unaingia Kuomba muda wowote na Uombaji wako wamazoea

Mtu ANAOMBA kwa kuinga mtu sio Roho.

HASARA ZA MAOMBI HAYA
1;Kutokupokea
2;Kutokujibiwa

2:Tabia ya Maombi Ya Nguvu
Haya huwa Maombi Yenye Matokeo mtu Anaomba Akiwa hawazi nje ya pale anapoomba

Tabia hii huombwa na mtu bila Kuwaza au Kuinga Maombi Au Kuomba kimazoea

Mfano
Unaingia ibadani. Kuomba Unaelekezea Kile Uombacho Usitoke nje

Omba na Uombe katika Roho Mtakatifu


FAIDA YA MAOMBI HAYA
1;Kupokea
2:Kujibiwa

3:TABIA YA MAOMBI ZAIFU.
Maombi haya mtu Anaomba TU huku Amechoka huitwa Tabia Zaifu ya Maombi

MFANO
Unaomba huku umechoka unasizia haupo katika Hali ya Kuomba hiyo huwa Tabia ya Uzaifu

HASARA ZAKE
1;Kutokupokea
2:Kutokujibiwa

4:TABIA YA MAOMBI YA KUJITOA
Haya Ni Maombi utayaomba bila Kuambiwa Uombe Mwenyewe Utajiwekea utaratibu tu 

Mfano;
Mimi naenda mkesha Mimi nitafunga mwenzi unasimama mwenyewe Kufunga

Ni utaratibu utakaojitoa na Maombi

3
FAIDA YA MAOMBI YA KUJITOA
1;Utapokea
2:Utajibiwa



HITIMISHO 
Tunaitimisha Kusema Ansate Roho Mtakatifu Kulifundisha Vyema ndani Yangu Basi Tusimame vizuri nakutafakari nakuandika SoMo Letu la Maombi Limeishia Hapa 

✍️ SEMINAR ✍️ TOPIC; MAOMBI ✍️VETA DAKAWA 2020 https://mchungajirichardi.blogspot.com/2020/08/seminar-topic-maombi-veta-dakawa-2020.html




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.