SOMO:KIJANA MKE MWEMA HATAFUTWI HULETWA NA MUNGU
☺️☺️SOMO😊 KIJANA MKE MWEMA HATAFUTWI HUTAFUTWA NA MUNGU.
Tufunue Vitabu hivi;
Mwanzo;2;20-24 Mithali;19;14 Ruthu:3;11 Mithali:31;8-10
Siku Zote kitu kilicho chema huwa kazi Sana Kukipata na kukiona endapo utatumia akili zako au wewe usiwe na Sifa ya kumiliki kitu chema huwezi Kukipata Utapata kinachofanania au kukaribiana Lakini Ukifata hatua Hizi Kama Upo kwenye Utafutaji wa Kuoa/Kuolewa Utapata MKE sahihi muda sahihi Na Ataletwa Na Bwana Wala wewe hutahagaika Kupoteza Muda wako Kutafuta Bint wa Kuoa au Mme wa Kukuoa.
Karibuni Vijana mjifunze kitu.......
DARASA hili linalenga Vijana wakike na wakiume Ambao wanafikiri MKE mwema/Mme mwema hupatikana kiurahisi kwa akili ZaKo Ni ngumu Sana kumpokea Endapo Akili Yako ikiwa imemshikilia mtu.
Kwanza Toka Mwanzo Adamu Alipofikia Umri wa Ujana Wake Anataka Kuoa Mungu Alimpa Usingizi mnono nakumletea mwanamke Kupitia ndoto na Baadae alimpata Eva Kama maono yake yalivyokuwa Adamu Alipita Hatua Zipi Tunazopaswa Vijana Tuinge.
1;HATUA YA KWANZA; ADAMU ALIMTAFUTA MUNGU AKAWA BIZE NA MUNGU.
Mwanzo;2;20-23
Tunapaswa Vijana Tutambue MKE mwema Kama anatoka Kwa Mungu Basi hatutampata uchochoroni au Sokoni Au Fiesta au Kwenye Basi Nk
Tutampata katika mazingira ya Mungu yaliyo na utukufu na Mungu nahutatumia nguvu zako kumshawishi au Kumpata au Kumweleza Mungu KILA Kitu Atahusika Kuwaunganisha.
Kazi ya Mungu humtaka mtu amtafute Kwanza Mungu uwe na Misingi mizuri ya mahudhurio Yako ya Ibada kanisani utoaji wa Zaka ya Fungu lakumi Kwako wewe kijana wa kike na wakiume.
Mme mwema au MKE mwema huwezi Kumpata mazingira yaliyo nje na utukufu wa Mungu Ukasema huyo umepata mme mwema/MKE mwema
Mbali Utakuwa umempata anaekaribia Kufikia hatua za MKE MWEMA.
VIJANA WA KIKE INGENI MFANO WA EVA ALIVYOMPATA MMEWE.
Bint wa Kike Hupaswi ukimbilie Kumpata mme nje ya mazingira ya Mungu yanayompa utukufu Mungu Wapo mabint wanakutana na kija uchochoroni au sted au Kwenye Basi au Kilabuni nk harafu Anasema na Yeye Amepewa Mme mwema Ndoa ikifungwa au kabla ya ndoa utashangaa Wameachana au Tayari Wamezini.
Eva Alikuwa mtu wa maombi Sana na hata alipotaka Kuolewa alimuomba Mungu Ampe mme mwenye hofu anayempenda Mungu Aliyemchungaji Mungu Alimtazama Eva akaona Anasifa ya Kushika Huduma ya Adamu ili Taifa la Mungu liendelee
Eva hakuwa Anajua Kama ataolewa na Adamu Lakini Mungu alivyowakutanisha wakawa kitu kimoja Sifa Hizi Zinaumbika ndani Yenu
1;Upendo Zaidi ya Upendo
2;MSAMAHA
3:Ansate
Mfano wa Eva Ndio unapaswa Bint wa Yesu ujue kumtafuta Mungu Usiwe mvivu wa ibada na Zaka ya Fungu la kumi.
Ukienda kinyume na Happ ndio Utapata wanaume Facebook au Sted au Sokoni ambao Mara nyingi huwa Wanahofu ya Mungu lakini kubadilika Ni muda wowote sio Kama chema.
2:HATUA YA PILI: ADAMU HAKUOA BURE BINT USIENDE KUKAA NA KIJANA BILA MAHALI UNAMUABISHA EVA MWEZENU Hakujirahisha hivyo uthamani wake.
Mwanzo;2;18-21
Adamu hakumpata Eva Bure Aligharamia Kwa Kupewa Kazi na Mungu ya KUWAITA wanyama Majina Wadundu mmea nk
Hiyo kazi ilikuwa ngumu Adamu mpaka alikuwa Anachoka Adamu kwakua aliitaji Apate MKE Aliwapa Majina Yote kila kitu unachokiona Leo
Biblia inaweka wazi hakupata jina la kuita MKE mwema au ubavu wake Mungu ndio Alipompatia Eva kuwa MKE wake.
Kama MWEZAKO Eva Adamu hakumuoa Bure au Eva hakwenda Kusema Kumsaidia Kuwaita Majina wewe Kwanini Unataka ujioe kiurahisi Unarusu unakaa na MWANAUME au Unazini nae kabla.
Kina Adamu tupo wengi lakini Nyoka Wapo wengi ndio Sifa Zao Nyoka nikuzini. Na Bint usipokuwa na Msimamo utajirahisisha kuzini.
3:HATUA YA TATU; ADAMU ALIKUWA VIZURI KIROHO MACHO YA ROHONI;
Unapotafuta MKE mwema kijana uwe na macho ya rohoni ya kuona Huyu Ni MKE wangu Mara nyingi katika jamiii yetu ya kitanzania Bint huwezi Kumfata mme Ukasema wewe mme wangu ndio maana Tunasema MKE mwema Anayemuona Ni Kijana wa Kiume yule anaeletewa Ndani ya Bint Mungu huunganisha TU haina haja yakutumia nguvu
Mfano::Adamu ndio alimuona Eva Na akajua Huyu ndio MKE wangu sio Eva alimuona Adamu(rejea;Mwanzo;2;23-24
4:HATUA YA NNE: AKILI NA UFAHAMU WAKO UWE VIZURI;
MKE mwema kumpata Akili Yako na Ufahamu uwe vizuri wakuweza kutambua Huyu Mwanamke atafaa Huyu mwanamme atanioa au Hapana
KIJANA Akili Yako na Ufahamu utulie unapochangua MKE mwema Katika ya mabint wengi atakaokuletea Bwana au Kukutana nao
Mwanzo:2;19-20
5;HATUA YA TANO; LAZIMA WOTE MUWE WATIIFU WA SAUTI YA MUNGU.
Hatua nyigine huwapasa mkae katika Hali ya Kuelewa Sauti ya Mungu Maana Sauti mtaisikia ikisema ndani Yenu Kama nyie Ni kusundi la Mungu.
Ni vyema mkatambua Sauti ya Mungu nakuweza Kuielewa Vizuri.
6:HATUA YA SITA: BINT HUWA HAPASWI KUENEZA HABARI ZA SIRI YA UPENDO WAO.
Hupaswi Bint Kutoka nje au Kutoa Siri zenu nje Hata Nani ndani ya ndoa hata ndani ya mahusiano Yenu Siri Uweke iwe Siri ya mmeo/mkeo
Kuna vitu vigine Ambavyo unatakiwa umwelezee mtu mwenye sifa maalumu
Watu wengi wamepoteza wanaume wema Kama Eva alivyorubuniwa na nyoka akatoa Siri ya Upendo wao siri ya mme wake nakusababisha mateso
Mungu aliingilia kumsamehe Eva lakini Mahusiano Yao yalitikisika kukawa Hakuna maelewano.
Bint wa kike/Kijana wa Kiume unapotoa Siri za Ndoa Yenu Uchumba wenu Ni Hatari kwenu.
Unapaswa Tunza Madhaifu ya MWEZAKO na mapungufu Yake usiyasambaze.
7;HATUA YA SABA: NDOA Hujengwa NA WATU WAWILI.
Ndoa inayokuwa na washauri na watu wengi ndoa hi huwa lazima Iwe na ndoa kwa Sababu ndoa imeletwa na Mungu sio Mwanadamu IPO siku utaabiwa huyo mkeo hakufai au mmeo nawe utamuacha.
Ndoa huwa inaitajika isimamiwe na Mungu mwenyewe ishauriwe na Roho Wa Ushauri hii itakufanya ndoa Yenu Iwe na Maisha matakatifu kinyume na hapo ndoa ikiwa inashauriwa nakusuhurishwa na watu au Unatoa Siri ndani Bint unapeleka kwenu au kwa marafiki ujue unajitengenezea ufa ndoa Yako njema.
Muache Mungu Ashughulike Alee Ndoa Yako Au Uchumba wenu mwachie Mungu.
Mabint Wengi Wamekosana na waume wao Wachumba kisa KUPOKEA ushauri mbaya.
Ushauri humuitaji mwanandoa ndoa Yake isiyo na Migogoro uwe unaifahamu amekaa miaka 5-10 kuilea ndoa ndio wakuomba ushauri
Mchungaji mwenye nguvu ya Kiroho na macho ya rohoni unayemjua nakumtambua Yupo hivyo.
Usiombe ushauri kwa kila mtu.na sio kila ushauri ufanye
HITIMISHO
Tunapaswa Tujifunze Mtiririko wa uchumba wa Adamu na Eva mpaka kwenda kuwa nafamilia Bora
Kupitia Somo Hili kwa nafasi Nimelifafanua ili uelewe
Wito
usijirahishe Kukimbilia kukaa na mwanaume kuzini nae
Kupata mme mwema MKE mwema yaitaji uvumilivu na utulivu Msimamo thabiti Kama Bint usijirahisishe kuwa Unazini zini.
Simu za maombezi+255759861768
@Pastor RICHARD 2020
Maoni
Chapisha Maoni