SOMO; UCHUMBA NA HATUA ZA KUOA KIBIBLIA
✍️✍️SOMO: UCHUMBA NA PROCESS ZA KIBIBLIA KUFIKIA NDOA✍️✍️
TUSOME Vitabu hivi.✍️✍️
Mathayo:5;37 Wimbo;4;1-5 Mithali;19;14 Luka;2;5 Kutoka:21;8
Hosea;2;19
✍️✍️ Karibuni Katika Somo Letu Hapa Leo Tutajadili na kujifunza Utaratibu wa mkristo Aliye na Uchumba Unaetaka Kuingia Kwenye Uchumba huwa kuna Process Zipi Kama mchumba uliyechumbiwa au Kuchumbiwa
Hatua Hizi Ni vyema Ukazitilia mkazo na maanani Kama Kweli Umeamua Kua ili kuurudi Ushuhuda wa Kristo na wengine kuinga kitu.
✍️Naekuletea DARASA Hili Naitwa Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richard
✍️DARASA LA Wanandoa
✍️✍️ UCHUMBA NI NINI..?
Ni process zinazopitiwa na jinsia mbili Mwanaume na Mwanamke zinazowapeleka kwenda kuwa Wachumba Wanaotambulika Au Kuingia kwenye ndoa.
Uchumba Ni hatua ya Pili ya kuelekea ndoa
✍️✍️ UMHIMU WA MKRISTO KUPITIA HATUA HII
Hosea;2;19
Mkristo anatakiwa apitie hatua hii ili kufanikisha ndoa iliyo na mpango sahihi ya Mungu.
✍️✍️HATUA ZA MKRISTO ZINAZOPASWA UFATE ILI KUKAMILIKA UCHUMBA ✍️✍️
A;URAFIKI.
Hii huwa hatua ambayo huitwa urafiki sababu nikipindi kinachowafanya wawili Hawa mjuane vizuri na kuchunguzana nakuwekana wazi nikipindi ambacho hampaswi mzini.
Huwa Kipindi hiki
_Hamtambuliki kwa wazazi wote
_Hamjaposana Wala Hamjajulikana kwa wazazi.
_Huzaa uchumba endapo urafiki huu Utakuwa mzuri.
_Huwa Kipindi hampaswi kukaa Karibu Karibu.
B;TAARIFA KWA WAZAZI UPANDE WA BINT.
Hi huwa hatua ya Juu Sana kwa walio marafiki hatua inayowatambulisha Kama wao Wachumba
Hatua Hizi hufatwa
1;Kupeleka Barua ya kishika uchumba kwa Bint(Posa)
2:Hutambuliwa Kama Wachumba pale Barua inapojibiwa upsnde wa Bint.
3:Uchumba hutambulika kwa wazazi
C:MAHARI
Hii huwa hatua ya Kuwapeleka kwenda kwenye ndoa.
Posa huwa tofauti na Mahali Posa huwa hairudishwi endapo Bint Atakataa Kuolewa na wewe.
Posa hutolewa ili wazazi wakutambue nakuyatambua mahusiano Yenu nyie wawili
Ukitoa Posa ndipo utakapopangiwa mahari na wazazi na ukoo wa Bint Kutokana na desturi za kwao.
Mahari sio Mpaka Pesa au Utoe Mali huwa Inawezekana wakakupa kitu kitakachokupasa ukifanye ili kuonesha umempenda Bint Yao unania ya Kuoa kweli.
Faida ya kufanya hivyo.
1;Kutimiza mpango wa Mungu
2;Kudhibitisha wewe unampenda Bint kweli.
3;Kuwa mmoja wa wanafamilia wa Bint
4:Kushukuru Kukutunzia Bint
5;Utaiheshimisha familia yako.
HASARA Usipotoa Mahari
1;Unatimiza Mpango wa Shetani.
Maana hata adamu alipewa kazi ya kuita Majina vitu Kisha ndio akapewa MKE mwema hakuoa Bure.
2;Unakosa udhibitisho kuwa Ni mkeo Halali
3;Familia inakutenga unakuwa si mmoja wa wanafamilia Bint.
4;Kwa upande wa Bint hutaheshimika.
Kwa hiyo kijana muoaji na Bint muolewaji Anatakiwa atoe mahali kijana ili Ajue alikugharamia naukija kukaa nae awe na uchungu hajakupata bure.
D:KUTANGAZA KANISANI
Hii hatua ukifikia hakikisheni mmeshamaliza taratibu kwa wazazi upsnde wa Bint
Kanisani Ni mhumu kwa mkristo KUTANGAZA uchumba wake Hii hufanyika kwa kushirikisha Hawa.
Hatua hii Mnatakiwa Tarehe ya ndoa Iwe inatambulika mtafunga lini ndoa na mkitoka hatua hii muingie Kanisani Kufunga Ndoa.
Bint unashauriwa na Kijana Kipindi Kama hiki ukae nao hawa
UPATE WATU HAWA KWA BINT na KIJANA ILI KUMSAINDIA
1;Watu waliokuwa vizuri kiroho na wananguvu ya Roho Mtakatifu wakuombee.
2;Upate Wanandoa waliodumu kwenye ndoa Miaka 5-10 Kaeni nao Hawa wawashauri msiende tu peke Yenu Kuingia ndani ya ndoa bila kukaa na wazee walio na muda kwenye ndoa.
3:Washirikishe Watu walio na Siri TU wasio wa mbea.
Ukifanya haya utafikia hatua vizuri ya ndoa.
E;NDOA
Hii huwa hatua ya MWISHO wa uchumba wenu na kuunganishwa na vitu vitatu
Upendo
Uaminifu
Imani
Hatua hii hukamilisha safari ya uchumba wenu
Kwa mkristo Unashauriwa.
-Funga ndoa kanisani usiishie kutoa mahari.
-Usifunge ndoa Serikalini isimame kanisani
-Usiwe na haraka kwenye ndoa muombee Mungu
-Usiongope gharama fanya ndoa ya uwezo wako ulionao.
F:MAISHA YA NDOA.
Hapa huwa mtiririko unaenda vizuri mkiwa na Pembe tatu.
Mke mmoja
Mme mmoja
Mungu mmoja
Ndoa Yenu itakuwa Yenye furaha.
Nawaombea Vijana Wote mnaojipanga Kuoa Mungu asimame nanyi.
@2020 Pastor Richard
Simu+255759861768 WhatsApp
Maoni
Chapisha Maoni