SOMO; UHUSIANO WA MUNGU NA KIJANA


✍️✍️SOMO✍️UHUSIANO WA MUNGU NA KIJANA:

;MWALIMU Pastor Richard
:@2020 Kanisa la Holy Spirit

✍️✍️YALIYOMO✍️✍️

1:UHUSIANO WA MUNGU NA KIJANA.
2;UJANA NA IMANI
3:INJIRI NA KIJANA
4:UCHUMI NA KIJANA
5:NDOA NA KIJANA
6: HITIMISHO

Nakukaribisha Kijana Ujifunze Jinsi Wewe ulivyowathamani na Mungu amezungumzaje kuhusu wewe kijana Nakala hii UTAJIFUNZA Mengi Soma kwa utulivu tu Nakala hii.

1; UHUSIANO WA KIJANA NA MUNGU👉👉IMeandikwa:Muhubiri;12:1

1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,Wala haijakaribia miaka utakaposema,Mimi sina furaha katika hiyo.

Kijana Anatakiwa Atengeneze UHUSIANO wake Na Mungu Akiwa Bado kijana Amfanye Mungu kuwa Kinga yake Amtumikie Mungu.

Kijana Anaweza kutengeneza Uhusia Wake Na Mungu Kwa Kufundishwa Neno la Mungu na Kulitii Neno linavyomuongoza nakutii ibada Yeye na Mungu muda kuuzingatia wa Kuingia ibadani na Kutoka.

IMeandikwa Zaburi;119:9👉Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako

KIJANA ASAFISHE NJIA ZA NA KUMTII MUNGU WAKE NA APENDE KUSHIKA NENO LA MUNGU SIO KUSIKIA ANALIACHA.


2:UJANA NA IMANI👉👉IMeandikwa;Muhubiri;11: 9;Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

KIJANA Anatakiwa Aufurahie Ujana wake Anapotembea TU katika maisha ya kumjua Mungu Maisha ya imani na Mungu.

Lakini Kijana anaefurahia kuishi maisha ya bila kuokoka nakumjua Mungu ajue mwisho wa hayo Ni hukumu Kutokana kuwa alifurahia kuishi maisha bila Mungu.

Muhubiri Anatuambia Ujana unapita Imani haipiti Heri kijana aliyepokea imani yakuchukia Ujana na Anasa zake.


3:INJIRI NA KIJANA 👉👉 IMeandikw 2:wafalme;9;4" Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Ramoth-Gileadi

Mwanzo;21;20

: 20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde

KIJANA Anapokuwa Ameamua kuihubiri injiri humtumia katika viwango vikubwa na kuwaleta watu wengi kwa Yesu na Vijana wezake

Mungu humimina nguvu na kumshika mfano wa Vijana walioinuliwa Kupitia Kuihubiri injiri 

Yeremia:Daudi:Yusufu:Yoshua:Isaka:

Hawa watumishi waliaza Kuihubiri injiri wakiwa Vijana na maisha Yao yalibarikiwa Kupitia injiri.

4: UCHUMI NA KIJANA 👉👉 Imeandikwa Mathayo;19;22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi

KIJANA Changamoto Kubwa inayomfanya Asikae na Mungu Ni Mali Maisha ya kijana Mara zote yanaangalia Mali utajiri na hazina za hapa Dunia Hii imekuwa Tatizo kwa Vijana.

Nini wafanye au wakichukulie hatua

1:Biblia inasema mtumikie Mungu na Mali zako maana yake Ni Pesa na Mali zisikutenge na mbigu

2;Kijana atambue umhimu wa Mungu kwake

3;Kijana afanye MAAMUZI yatakayomfanya Mungu Azidi kubariki kazi zake.

4:Kijana Asiwe busy katika Utafutaji kuliko Mungu

5:Atenge muda wake na Mungu

6;Afanye moyo wake umuone Mungu kabla ya Mali.


5:NDOA NA KIJANA👉👉Imeandikwa;ISAYA;62;5;Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe

KIJANA Biblia inamwelezea kijana wa Kiume macho yake anapoona Bint Mzuri 

Kama Vijana Tunapaswa Kuoa na Kuepuka vishawishi mbalimbali Lakini Kama unaona Vyema unaweza Kukaa maisha bila Kuoa sawa

Vijana wengi wanakimbilia Kuoa Au Kuolewa Bila Kumuomba na kushirikisha watumishi na hujikuta wanapata wake na wanaume Wasio mpango wa Mungu.

Na hii inasababisha ndoa nyingi za Vijana kuwa na migogano mingi na Kuvunjika kuachana na Kuumizana


Kama Vijana Tuliotengeneza uhusiano wetu na Mungu tuwe wavumilivu na Tumuombe Mungu Atatupa sahihi.


6: HITIMISHO ✍️

Mwisho Tunapaswa Sisi Vijana Tujenge uhusiano wetu na Mungu na Sio mambo ya Dunia sio Anasa Mali na ubusy wa Kukosa muda kumtafuta Mungu utatupeleka Pambaya.


Kwa msaada wa KIROHO na Kuokoka Piga simu Pastor Richard Jioni+255759861768

Neno Nawaachia👉👉Mithali;7;1;Mwanangu, yashike maneno yangu,Na kuziweka amri zangu akiba kwako

@2020Pastor Richard

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.