SOMO; DALILI HIZI NDIYO UTAJUA MAHUSIANO YENU HAYATADUMU

⛏️⛏️DARASA LA WANANDOA⛏️🔨🔨

SOMO; DALILI TANO KUMBWA ZA KUJUA MAHUSIANO YENU HAYATADUMU UKIONA DALILI HIZI. Chukua hii mwanangu tahadhali.

Soma Mithali;7;6_10 Mithali;12;4 Mwanzo;2;24

Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard

Yupo Morogoro veta Dakawa

Simu+255759861768

🔓🔓Kuna vitu unavyotakiwa uwe navyo makini katika ndoa yako mahusiano Yenu maana huwa chazo kikubwa Cha mahusiano kuvunjika au kutokuendelea katika mafanikio au hatua Mambo haya matano Ninaenda kuyafundisha.

🔓🔓 DALILI HIZI HUKUJULISHA MPENZI ULIYE NAE HUTANDUMU NAE

1;MPENDA PESA

Ukiona mpenzi wako Anataka au kupenda pesa Kutoka Kwako au Anakuomba Pesa bado hamjaoana mpo tu uchumba KILA mmoja kwao ujue uchumba wenu huo hamtandumu Kutokana Mwezako kakupenda kwa ajili ya Pesa na unavyompa Pesa

2;MUONGO

Ukiona mpenzi wako uliye nae anakudaganya Mara kwa Mara na ukijua anakuambia nilikuwa nakutania au Anakuambia kweli kabisa wakati unajua anakudaganya ujue Ni dalili tosha kukujulisha sio Mwaminifu Kwako na hakufai unatakiwa achana nae.

3:HANA MUDA NAWEWE.

Ukiona mahusiano Yenu hamna mawasiliano mazuri hamuongei vizuri au hamuonani hata Mara Moja kwa wiki KILA mmoja Yupo busy ujue mahusiano Yenu yanaenda kuvunjika

Mnachotakiwa mpate muda wa Kuonana na kuwasiliana endapo mpo mbalimbali lakini Kama mpo KARIBU tengeni muda wa kuongea na kukaa Pamoja.

4:HUUDHI KILA MARA.

Ukiona Mwezako KILA wakati anakuudhi ujue hiyo Ni dalili ya kwenda kuachana mmechokana na Anaamua anakuuzi ili muachane NAWEWE kwakuwa hujui umeg,ag,ania TU wakati kumbe Mwezako kakuchoka.

5:ANAKUZA JAMBO

Ukiona Mwezako ukikosea hakusamehi au hakujulii Hali ukiumwa au anayakuza nakuyachimbua yaliyokuwa yamepita nyuma uliomkosea ujue mahusiano Yenu hayadumu yanaishia njiani muachane

🗝️🗝️KAMA UPO HIVI YAFANYE MAHUSIANO YAKO YADUMU.🗝️🗝️

Mahusiano unaweza Kuyafanya yadumu au Yasidumu Ni wewe mwenyewe

KARIBU ujenge mahusiano na ndoa inayodumu acha kuanzisha Misingi ya uchumba usiodumu.

1;UKWELI NA UWAZI

Hakikisha humfichi na unamweleza kweli yule uliyempenda Kupitia kujua UKWELI yeye ataamua akuache kwa kuwa amekujua ukweli au aendelee na wewe.

Mnapoanzisha uhusiano weka wazi Mambo yako mkija kuishi wote mweleze kweli mwezako

Mpenzi mwema AMBAYE Ni wako hawezi kukuacha ukiona Amekuacha ujue sio Mmeo huyo.

2; NAKUPENDA

Tumia Neno kulitamka masikioni kwake asikie Neno "Nakupenda Sana" Neno Hili hubadili hisia za kukuchoka nakujihisi anapendwa na kujaliwa fanya hivyo utayadumisha mahusiano yako.

Tumia maneno mazuri Yenye mvuto wa kimahaba usiwe kama chiriku au Unatamka Kama umepaliwa nachakula mdomoni

3:MUDA
Tafuta muda wa kuwa nae karibu na Mwezako Usikae muda mrefu bila Kuonana nae au kumtembelea utayahatarisha mahusiano yako

Tafuta muda kaa nae na mpange mikakati ya ndoa Yenu na Maisha Yenu

Usikae muda mwingi Upo mbali nae Fanya surprise ya kwenda kwake bila Kumwambia

Utayafanya mahusiano yako yadumu

4:AGANO

Tumieni Agano la uchumba Ukiona Mwezako anakataa kuweka Agano na kwenye uchumba ujue huyo sio Mmeo au mkeo

Agano la uchumba huwa lazima mfike kwa wazazi. Marufuku kuishia njiani bila kwenda kwa wazazi.

Hakikisha huzini nae mpaka mfike kwa wazazi na wazazi wamewapa BARAKA

5;ZAWADI

Mpe zawadi za kusuprice Mwezako Mara kwa Mara mnunulie nguo mnunulie Simu Mpe zawadi kitu Cha kukufanya atakukumbuka.

Vijana wa Kiume unatakiwa mnunulie mkeo zawadi Na mshonee nguo au kanga mfanyie hivyo Mara kwa Mara Vijana wakike mnunulie shati suruali Mwezako mfanyie hivyo Mara kwa Mara.

🎬🎬🎬UKIFANYA HAYA UTAYAFANYA MAHUSIANO YAKO YADUMU MPAKA NDOA MTAFIKA

Wafundishwe na wengine tuma kwenye group zako.

Naitwa Pastor Richard

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025

KITABU IJUE NDOTO YAKO