SOMO: UMHIMU WA MUDA KWA MWEZI WAKO
✍️✍️SOMO: UMHIMU WA KUWA NA MUDA NA MAWASILIANO KWA MMEO/MKEO✍️✍️✍️Chukua Hii Ufurahie ndoa Yako.
✍️✍️DARASA LA WANANDOA
✍️✍️MWAL; PASTOR RICHARD
✍️✍️Simu+255759861768
Mithali;14;1-2 Waefeso;5;21-24
MUDA na MAWASILIANO ni vitu ambavyo vinahitajika Sana kwenye mahusiano Kati MWANAUME na Mwanamke hata Kama mnaishi mbalimbali au nyumba Moja Muda wako kukaa kwa ajili umpendae au Kuongea na kuwasiliana Ni Mambo yanayoweka hai mahusiano Yenu.
~MUDA utakufanya umfahamu vyema mwenzio ikiwemo kipi anapenda na kip hapend
~MAWASILIANO yatakuweka Karibu nae haijalishi mna umbali kiasi gani uwepo wako utaonekana, pia ktk mawasiliano jengeni muda wa kuongelea mahusiano yenu na yale msiyopenda yatendeke baina yenu
TUMIA MANENO HAYA MATAMU KUJENGA MAHUSIANO YA FURAHA NA AMANI
1. NAKUPENDA~Weka hisia zako wazi haijalishi mmekuwa kwenye mahusiano kwa muda Mrefu mwambie Mara kwa Mara mtext mwambie hata anapokuwa kazini.
2. MSAMAHA~Kuwa mwepesi wa kuomba samahan unapokosea tengeneza mapatano na Aman kwa maana Aman inapotoweka ndani Kuna Baraka zinapotea pia, hata ww mwanaume omba MSAMAHA unapomkosea mkeo
3. KARIBU mme wng/Mke wng~ Ni furaha Sana anapokuja eidha toka kazini au safari unapomkaribisha kwa Upendo na tabasamu kumpokea,kumuwaooo
4. POLE mme/Mke wng~ kutwa mzima watu ukutana na makwazo mbalimbali ila tuhakikishe kila mmoja hasibebe makwazo ya nje kuleta ndani mfanye Mke/Mme kuwa tulizo na siyo kumtwika upweke kwa kumnunia.
Tumia Maneno Haya Manne Kwa Mkeo/Mmeo Utaifanya ndoa Yako iwe Yenye furaha na Amani
HAKUNA MUHITIMU KWENYE NDOA NDO MAANA VYETI VYA NDOA VINATOLEWA KABLA YA MAISHA YA NDOA IVYO MAISHA YA NDOA NI DARASA AMBALO UKINGO WAKE NI MAUTI KILA SIKU WANANDOA NI WANAFUNZI.
NI KWELI AU SIYO KWELI?
Comment na SHARE mafundisho haya
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni