SOMO✍️✍️ NGUVU YA KUDHIBITI MAPITO
✍️✍️🌱🌱SOMO✍️ NGUVU YA KUMTENGEMEA MUNGU KATIKA KIPINDI CHA MPITO✍️✍️🌱🌱
Tufunue Biblia Zetu Zaburi:91;7-16✍️Zaburi:89;24-26
✍️✍️DARASA LA NENO LA MUNGU
✍️🌱🌱MWAL; PASTOR RICHARD
Nipo Morogoro veta Dakawa
✍️✍️UTANGULIZI✍️✍️
Kuna wakati unaweza ukawa unapitia mapito Magumu Sana na wakati Mgumu Sana Mpaka hata nguvu ya kuendelea kuomba inaisha nguvu ya kumtafuta Mungu inaisha.
Ujue Ukiwa katika Kipindi Kigumu ndio wakati wa Kumwita Mungu Aitike Ndio wakati unaokupasa wewe umuaibishe Shetani na uaibishe wakati huo wa pito
Leo hii Nataka ujifunze nguvu ya Kumtengemea Mungu wakati wa mpito na Magumu Utapataje nguvu ya kuendeleaa mbele kusitahimili vipindi mbalimbali Utapataje.
KARIBU Naitwa PASTOR RICHARD Kama ndio Mara ya Kwanza Kunifatilia kwenye ukurasa wangu wa Moto wa Yesu fb na Sehemu zingine Masomo haya yanapokufikia
Simu upige Jioni ya Maombezi+255759861768
✍️✍️ LENGO Kuu la.Somo; Ujifunze jinsi ya kudhibiti mapito Kwako yasiyoyalazima
✍️✍️Dhima Ya Somo✍️Ni kuandaa watumishi wenye nguvu ya Kumtengemea Mungu
✍️✍️MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOPITA KATIKA KIPINDI KINGUMU✍️✍️
1:Anza kujifunza kwanini imekupata Hali hiyo chazo Ni Nini upitie mapito hayo.
2:Jiridhishe kuagalia mwanzo wa Tatizo Kisha Anzia pale lilipoanzia kulitatua
3:Shirikisha Wanamaombi wezako Baba yako wa Kiroho Kisha Anza kuliombea
4:Jipe matumaini mwenyewe kwa Kusema nitashinda na imekuwa hivi kwangu sitabaki nilivyo Sasa.
5:Mwendee Taratibu umweleze Anayesababisha Tatizo Aache kukufatilia.
6;Kuwa na Imani katika maamuzi yako Upo sahihi
7;Usiangalie mtu yeyote au wazazi au mtu flani atanisaidia Fanyia kazi msimamo wako na Jisimamie mwenyewe na kujicotro katika matumizi ya pesa.
8;Waache marafiki wasiokushauri na kukuongoza katika Mungu.
9;Wachumba na mahusiano yasiyo na mwelekeo au dira yoyote yavunje uazishe mahusiano Yenye mwelekeo na dira.
10:Epuka kujihusisha na Mahusiano au Makundi endapo bado hujaweka mwelekeo wa maisha yako au hujajitengemea.
11:Toka kwa wazazi au mazingira uliozoeleka toka utotoni nenda Mkoa au sehemu nyingine ukaanze maisha yako.
12:Puuzia Ushauri mbaya au unaokutenga na Mungu mpende Mungu na kumtii.
13;Upende kujifunza vitu mbalimbali kusoma Vitabu mbalimbali nakala mbalimbali utaendelea Kupata Ufahamu
14:Kuwa na Mtu wa KARIBU Atakayekushauri nakukuombea nakufanya nae kitu pamoja kuwa na mtu aliyekaribu Ni faraja atakutia moyo.
15;Tumia Simu yako kubwa kujifunza mambo njia mbalimbali na Masomo mbalimbali Shuhuda mbalimbali nk
16;Usikae nao waliojikatia tamaa au wanaongelea ya Dunia mfano vijiweni kwenye fullpulo mipira nk.
17;Tunza muda wako nafanya Mambo yako kwa kufata muda jali muda wako usipoteze Miaka Upo vile vile.
18;Weka Malengo yako yawe na muda nayatimie kwa Muda ulioupanga.
19;Usiishi kwa kuinga maisha ya Mtu ishi Kama Mungu alivyokubariki.
20;Ridhika na kila Hali kila mazingira yoyote ishi.
✍️Hitimisho✍️✍️
Haya ndio ya kuzingatia Unapopitia changamoto na kuepuka mapito yasiyolazima au yakujisababishia wenyewe
Tunapaswa Tujifunze Kutunza Muda na tujiwekee mipaka mwisho muda au mwaka fulani nitafanya hivi tukitunza Muda Tutaenda vizuri na umri wetu hautatupa mkono.
✍️✍️WITO WA SOMO✍️✍️
Watumie Ndugu jamaaa marafiki kwenye group zako na Facebook
Maoni
Chapisha Maoni