✍🏾✍🏾SOMO:PUPA
✍🏾✍🏾SOMO:PUPA(Usiwe na Pupa)
Tufunue Biblia Zetu Tusome ✍🏾✍🏾Mithali;21;5 Mithali;23;18-23
✍🏾 UTANGULIZI✍🏾
Leo Nataka niwafungue watu wafanyao vitu kwa Pupa bila Ustaraabu wao popote pale wanapofika wanaile Hali ya kufanya vitu kabla hata wenyeji hawajawakaribisha Yeye muda Ameshapazoea Mpaka chumbani na hata katika kula hajanawa au Kuomba Yeye Ameshaanza Kula watu wapo ambao nyumbani kwao walilelewa kutokuwa na Ustaraabu katika pale wanapofika sehemu yoyote ile Mungu Watu Kama hao hafurahii Mtu Ambaye Anakula chakula Kama kinaisha au anakunywa soda Yupo ugenini Mpaka wenyeji ukiondoka unawapa Maneno yakuongea
Fanya kila Jambo Kwa Ustaraabu usiwe na pupa Popote unapoenda Hii Hali itakupa heshima ya Ustaraabu Usifanye vitu ovyovyo au shaghalabagala Fanya Kitu hata mwingine anaekutazama Aseme Mtoto wa fulani anautii na heshima si mmemuona hafanyi vitu ovyo ovyo unapokuwa Unafanya vitu bila Pupa unajitengenezea Sifa Nzuri kwanza kuwa Unafanya Mambo kwa utaratibu.
Karibuni Katika SoMo Hili Limeandaliwa na Kuletwa Kwenu Na Pastor Richard kwa uongozi wa Roho Mtakatifu.
MAKAO MAKUU Morogoro veta Dakawa.
Pupa Ni Nini?
Pupa Ni kufanya Mambo yako bila kufikiria.
HASARA za KUWA NA PUPA
1;Huwezi Kuendelea mbele Kama Unafanya Mambo kwa Pupa
2;Utakuwa hufikiri vitu vya kufanya Kutokana Na roho ya Pupa
3;Vitu vyako haviwezi kudumu Kutokana uliviazisha bila kufikiri.
4;Unakosa Ustaraabu na Kuaguka katika maamuzi yenye Hasara.
FAIDA Utakazopata UKIACHA PUPA
1;Watu watapenda Tabia yako nakuiga Tabia hiyo.
2: Utafanya Yenye faida katika maisha yako
3:Utaongozwa na Maamuzi yenye faida katika maisha yako
4;Utaendeleaa na Kufikia ndoto zako
WITO WA SOMO LETU
Linalenga kutubadilisha tuchukie pupa na kufanya Mambo kwa Ustaraabu Hali itakayotufanya tusijutie maamuzi Yetu.
Hitimisho
Tuombee
Baba Tunaomba wanao Utupe roho ya Ustaraabu uondoe pupa ndani Yetu katika jina la Yesu;Amen
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni