Somo: VUKÀ

🌳🌳SOMO; NJISI YA KUVUKA ULIPOSHINDWA KUVUKA✍🏾✍🏾🌳🌳🌲🌱🌱
Tufunue Biblia Tusome vitabu hivi
Mathayo;14;34 Matendo:18;27 Hesabu;32;30 Torati:9;1-5 Yoshua,;3;1-17

🌳🌳🌳 UTANGULIZI🌳🌲🌱🌱

Shalom Wanangu Karibuni Neno la Mungu kwa uongozi wa ROHO MTAKATIFU Somo Linaloenda Kukuvusha Hapo ulipokwama kuvuka Hakuna mtu aliyekuja kukutoa hapo lakini Kupitia Neno TU unaenda kuvuka Yordani unaingia kanani.

Naitwa Pastor Richard Ni Mwanzilishi wa makanisa ya Huduma Ya Roho Mtakatifu Tanzania (Holy Spirit Ministry Tanzania) Makao makuu Morogoro veta Dakawa Huduma hii inalenga Ukombozi na Mafundisho ya Neno la Mungu Katika uongozi wa ROHO MTAKATIFU yenye kukufungua na Kukuponya katika fikira na mawazo ya elimu ya shetani na kukupa elimu yenye uwezo wa ukiungu ndani Yako katika Kufunguliwa Kutoka kwenye matatizo

Lengo La Somo la Leo Unatakiwa Uende hatua nyingine sio kulia Lia wakati farao na jeshi lake wanakuja nyuma.

KUVUKA NDIO KUFANYAJE.

Ni Hali ya wewe Kutoka katika Hali ya kushindwa kwenda kuweza kulitawala Jambo au kumiliki vitu ulivyokuwa umeshindwa kumiliki.

Vuka; Toka sehemu ulipo uende sehemu palipo nafasi Yako Acha kuona huwezi

Tunapozungumzia Kuvuka au Vuka Namanisha Kuna wakati Mtu Anaweza akawa anashindwa Kupokea majibu kulingana na mtu kujiona amekwama kuvuka

Mfano mzuri Tunaangalia
Wanaisraeli Walipotoka misiri waliendelea kusonga vizuri lakini Baada ya kufika mbele wakaona Bahari walianza kumunug,unikia Musa yule aliye kuwa anawaongoza katika msafara wa kuvuka Kutoka kwenye  Mapito na Matatizo Yao walichoanza kuongea Musa Musa umetuleta huku ili utuue kwenye Maji haya au Bahari hii ulijua kabisa huku Hakuna njia ukatuambia Kwa Mungu kunaraha na Tunaenda Kutoka kwenye matatizo walianza kumlaumu mchungaji wao Musa aliyewatoa misiri.
Musa na yeye aliona Bahari na hicho ndicho kilimfanya amuombe Mungu amlilie Mungu Lakini Mungu hakushuka aje awavushe isipokuwa kumuuliza Musa Akamuuliza Unanini Mkononi mwako Musa akasema Anafimbo(mamlaka) Nyosha fimbo hiyo yapinge Maji alifanya hivyo njia ikaonekana walio kuwa na Imani walivuka waliokuwa wanasitasita waliendelea kuona Maji na Jeshi lilipofika waliuawa wale waoga wenye kusitasita wezao waliona njia Kwenye Bahari wakavuka Lakini Cha Ajabu Jeshi la farao walipoanza kuwafata walikuwa hawaoni njia wanaona kuzama TU wakafa wote

Maana Yangu USHINDI au ILi uvuke hapo lazima Kama upo katika Mapito fulani usione pito ona kwenye wazo lako hauna pito

Ukitaka Utembee juu ya Bahari kwa Imani lazima usione Maji mbali uone nchi kavu

Ukitaka Utembee katika kulipa madeni lazima uone utalilipa Deni sio uone hutalipa Deni

Ukitaka Utembee ndani ya ndoa ya Amani lazima uone ndoa Yako inaamani.

Usiwe Kama Petro Unajua Ilikuaje
Petro alimuona Yesu anatembea juu ya maji(Kwenye majaribu) lakini Yesu alikuwa haoni majaribu au Pito yeye alikuwa Anaona Yupo Anapitia wakati wa kawaida TU yaani Yupo nchi kavu sio majini Petro mwenye imani ya kuona Yupo kwenye maji Alimwambia Bwana nije nikufate Yesu Alimwambia Njoo Petro kuanza Kukanyaga TU maji Akaanza kuzama Kilichotokea kumuita Yesu Yesu niokoe nazama Yesu akanyosha mkono
Na kumuuliza Imani Yako iko wapi Sasa.

Na Manisha wapo watu wanatabia Ya Petro Kama aliyokuwa nayo alikuwa Anapenda Asimame Na Yesu lakini alikuwa Anashindwa kwa Sababu alikuwa Anaona tofauti na Mwalimu wake Hebu fikiria Petro anaulizwa huyu Ni Mmoja wa wanafunzi wa Yesu Akamkana Yesu kwa kuwa aliona kwa macho Yake amekamatika ndio Mwalimu wangu Mimi ndio kabisa wataniua

Acha kuona Kama Petro Ili upavuke hapo Kama Utaendeleaa kujiona unavyojiona maisha Yako hayatafunguliwa.

Acha kuona huna kazi uone unakazi

Ukitaka upate Mtoto jione unamtoto sio huna Mtoto.

Hebu mwambie mtu Mmoja ona Unavuka hapo sio uone umeshindwa.

Naitwa Pastor Richard

Simu+255759861768 piga njioni

Morogoro veta Dakawa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.