SOMO; SAUTI YA MUNGU Sikia

✍🏾✍🏾🔥🔥SOMO; SIKIA SAUTI YA MUNGU NAFANYIA KAZI SAUTI HIYO🔥👏🏽👏🏽
Tufunue Biblia Zetu Tusome Vitabu hivi
✍🏾1Wafalme:18;23-43✍🏾1Samweli:8;7-23' 28;12-23🔥Mwanzo;3:8-17

         ✍🏾✍🏾🔥 UTANGULIZI🔥🔥👏🏽👏🏽

Sauti ya Bwana au Sauti ya Mungu Ni Sauti inayokuijia kwa malengo makuu manne TU
1:Kukuonya
Utaona wazo au fikira ndani yako zinakuja Kama zinakuonya na kukemea uache bila kukupa Sababu au maelezo mengi

2;Kukuongoza
Utaona wazo au fikira zinakuja zikikupa mwanga Nini Ufanye na Kukuelekeza uende wapi kanisani ukaongee na Mchungaji au ufanyaje.
Sauti hiyo haitakuwa na sababu au maelezo mengi.

3;Kukueleza
Utasikia wazo au fikira inakuja kwa njia ya Kukuelekeza Nini Ufanye njia na madhabahu itakayokuponya au Tatizo lako Lilivyo Sauti itakuelekeza

4;Kukufundisha
Utaona unapewa elimu juu ya ulichokuwa hikijui Kupitia wazo lako au fikira

Zote point Nne zinasimamishwa na 2Wakoritho:10;5

Wapo watu wamekuwa wakizitii nakumfata Shetani Sauti ya Mungu ndani Yao hawaielewi Narudia Kusema Sauti ya Mungu itakuijia katika Fikira Zako au Mawazo Yako Njisi utakavyoilewa kuwa hii Ni Sauti ya Mungu Mawazo yako yatakuja yasiyo na sababu katika Maamuzi yako ukiona Unatoa sababu ujue Ni Sauti ya Shetani au Ukaona unaambiwa omba Unaanza kukumbuka dhambi zako au uchafu wa matendo yako  ujue unasikiliza Sauti ya Shetani.

Karibuni wanangu Tuendeleee Naitwa Pastor Richard Naekuwasilishia SoMo Hili

Lengo la Somo Tufanyie Kazi Sauti ya Mungu Ili Tupone.

Walengwa wa SoMo KUANZIA umri wa kuanza kujitambua na watu wote wenye akili timamu waliokoka na wasiokoka

Somo Hili litakufungua Shetani asikuambie Zini eti utatubu dhambi hiyo Au Toa mimba kwa Sababu hujajipanga au Siendi Kanisani kwasababu mbali Yaani ukiona katika Maneno yako Unatoa sababu Basi utabue uendacho kukifanya au Kukiamua umeamuriwa na Shetani na sio Mungu.

UKIONA Unaambiwa Mpigie Pastor Richard mweleze Pastor Richard au Nenda Kanisani au Usizini au Tubu dhambi ya umbea au Samehe kila Mara linakuja wazo fikira au ndani mwako unasikia Sauti isiyokutazamisha madhaifu yako au Kukupa sababu ujue Ni Mungu Anasema nawe Tii na Ufate utapokea Ushindi.

Hasara Kupuuza Sauti ya Mungu

1;Mungu kunyamaza asikutumie au Kukujibu
2:Hutaelewa chochote kila Kitu Utakuwa kipofu.
3:Hutaona Matokeo ya uombacho
4;Imani itasombwa na pito
5;Utaendeshwa na mawazo ya kipepo TU
6;Utakuwa Mungu Sauti Yake unapuuza
7;Utakemea majibu yako
8; Utaendeleaa Kukumbuka madhaifu
9;Utaendeshwa na dhambi fulani
10:Utapotea katika usahihi pa kusimama nk

Faida ya Kusikia Sauti ya Mungu

1;Kuelekezwa
2;Kuongozwa
3;Kutawala
4;Kumiliki
5;Kufundisha kwa usahihi wa kumfungua mtu.
6;Kutumika kwa Uaminifu
7;Kubarikiwa
8;Kuheshimishwa
9;Kuinuliwa
10;Kukua Kiwango Cha Imani ijibuyo
Nk

Dalili hizi zinakutenganisha na Sauti za shetani

Naitwa Bishop Richard
Morogoro veta Dakawa
Simu+255759861768

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.