SOMO; NYAMAZA
✍️✍️✍️SOMO; NYAMAZA
TUNAMSHUKURU Mungu kwa Neema Zake na Rehema
Leo hii Tumekutana Tena Katika Kukumbushana nakufundishana Neno la Mungu Leo Tunajifunza Neno Nyamaza ✍️✍️
🗨️🗨️Vitabu:Kutoka:14:12-20✍️ ISAYA;36;21✍️42;14✍️Amosi:5;13✍️✍️Zaburi:39;5-10✍️Mithali;17;28.
✍️✍️✍️🙏 UTANGULIZI 🙏🙏✍️🙏
Hata Mpumbavu akinyamaza Asikujibu akaa Kimya huitwa mwenye hekima Lakini mtu mwenye hekima Anaweza akaitwa mpumbavu kwa kuwa tu ajui kunyamaza Anajua kujibishana Tu Anakinywa Ambacho hakiwezi kukaa Kimya Yeye Anaweza kuongea na kupinga kelele mpaka majirani wanakuwa Sasa mpaka wanamchoka. Kumbe jibu la kunyamaza na kukaa Kimya huwa siraha tosha kwa mwenye Hekima.
👉👉 NYAMAZA WE ADUI Kuna Wakati Tunapaswa Tuvinyamazishe Kila magonjwa hofu Laana mikosi na vijiinuacho mbele Yetu Sasa Ili Tuvinyamazishe Tunatakiwa Tuwe na NGUVU YA IMANI
Tusiache Mambo yazidi kujiinua bila Kunyamazishwa yatatutesa Tumepewa JINA LA YESU
Hupaswi uongope au uhofu ukiwa Imani yako umeijenga juu ya JINA LA YESU
👉👉ACHA MUNGU ASHUGHULIKE usiaze kumsaidia Mungu au Kuaza kujitetea mwenyewe katika pale unaposhindwa kaa chini Uagalie nyuma na ukumbuke aliyokuvusha Mungu KiSHA JISEMEE NITAVUKA NA HILI
Naitwa Bishop Richard Karibu tuendee na Somo Letu
👉👉 MAANA YA KUNYAMAZA; Kukaa Kimya usiongee Kitu
👉👉LENGO KUU LA SOMO; Kutambua nguvu iliyomo katika Kunyamaza
👉👉WALENGWA; wanawake na wanaume wasiojua kunyamaza
Kuna watu ambao Mungu Ameshindwa kuwajibu kwa Sababu ya kutokujua kunyamaza utamkuta Kelele Yeye kunug.unika Yeye Hajawahi Kumwambia Mungu Shughulika mwenyewe Mimi nimeshindwa pito Hili Yeye anazidi kupambana nalo Tu Anaona Limemzidi Bado yumo Tu Mara hospital haponi Mara maombi hajibiwi Mara huku lipo pale pale
Unachotakiwa Anza Kumtumikia Mungu Tu na kujitoa kanisani halafu lile lilokutesa Mwambie Mungu Saivi Nataka Ufanye njia Nipite Mimi sioni pakupita Nakuomba baba halafu Amini unaenda kupita.
Wapo watu wanakosa na watu na kuchukizana nao kwa kuwa Hawajui kunyamaza Kila siku wanaonesheana ubabe aliyeokoka na ambaye hajaokoka ukiwakuta wanavyotukanana mpaka utachoka kumbe wewe nyamaza JIFUNZE kunyamaza Iwe kwenye ndoa yako Ili kuepusha marumbano na mijadala nyamaza TU Kama unamtu anakuandikia sms za Kutaka uaguke kiroho au kukutukana usijibu hiyo sms nyamaza Tu
Usiwe mtu wa Kujibu Kila kitu acha wakuone wewe mjinga kumbe unahekima
👉👉 FAIDA UTAKAYOPATA UKINYAMAZA
👉Kwanza Utashinda vishawishi vingi na Mitengo mingi ya Shetani
👉Utaifanya ndoa yako mahusiano yako yasiingiliwe na Adui au kuvunjika
👉Utamfanya Mungu Akupinganie ili ajibebee Sifa kwako.(Kutoka:13-17
👉mapito mengi Utayashinda
👉Utampa maswali adui yako nakumtia hofu.
👉Utamfanya Adui Yako Asikufatilie au kukusonga.
HASARA ZA KUTOKUNYAMAZA
👉Kwanza Utajikuta umeingia kwenye kishawishi na kutenda dhambi
👉Utamfanya Mungu akuache tu asijishughulishe na wewe.
Kutoka;14;14
👉Mapito na Changamoto ndogondogo na kubwa zitakuzidi uwezo.
👉Utampa nafasi adui yako akutese
👉Utamfanya Adui ndio Akufatilie na kukusongasonga
👉Utaharibu na kuvunja ndoa yako na Uchumba wako.
👉👉👉👉 HITIMISHO👉👉👉
Tunapaswa Tujifunze kunyamaza tutashinda mapito mengi
Tuombee Pamoja
Baba katika jina la Yesu Tunakuja mbele zako Tumekukosea katika vinywa vyetu Tumengombana na watu Kupitia kutokunyamaza lakini Leo hii umetukumbusha wanao Tujifunze kunyamaza tusijitetee wenyewe Roho Mtakatifu karibu utufundishe kuwa Tunanyamaza nalileta Kundi lako na wanao Baba ukafundishe wewe Wajue kunyamaza Katika jina la Yesu:Amen
👉👉👉WITO👈👈
Tutumie namba HIZI kwa wanaotaka kuokoka na maombi
Pastor Richard Jioni mpingie+255759861768
Kutoka Kanisa La Holy Spirit
Lenye Makao makuu
Morogoro veta Dakawa
Maoni
Chapisha Maoni