SOMO; MAISHA YAKO YAKAINUKE UPYA ADUI ZAKO WALALE CHINI YAKO

🌍🌎🔥🔥SOMO: MAISHA YAKO YAKAINUKE UPYA ADUI ZAKO WALALE  CHINI YAKO🔥🌴🌴🌴

Tufunue Biblia Zetu Natumaini Yu Mzima na Upo Fireee Bado Moto uliotoka nao Veta Dakawa Bado unawakaa Basi Leo Adui yako akainamishe kichwa chini yako Iwe Ni ugonjwa madeni mapepo kudharaulika;Kukatishwa Tamaa Maisha yako kupofuka Leo hii naamuru katika SoMo hili Ukainuke na nguvu mpyaa.

Zaburi;20;8 Nehemia;12;37 Nahumu;1;8 Yoshua:8;3-19
Luka;7;14-17

                     🌍🌎🔥 UTANGULIZI🔥🔥🌴🌴🌴
Kiukweli Tunapaswa Kuinuka na Kusimama Sio Kuwa Tunainuka Tunaanguka Tunainuka Tunaanguka Kwanini hatusimami Kwanini Tuteleze Tuanguke Nini Tatizo Tunaanzisha Vitu vinakufa havisimami Tumefungua cafe lakini saivi imefungwa Tumeanzisha duka lakini mtaji hatuoni Kwanini Hatusimami Tunaanguka Anguka Tumeokoka Lakini wengi Leo wamerudia dhambi Wapo Watu ndio kabisa kusimama wameshindwa Kabisa wana ndoto nzuri malengo mazuri Tatizo liko wapi Sasa Leo hii Shetani na Falme Zake ninamuamuru na kumuinamisha chini kichwa chake Iwe Ni roho ya uharibifu Iwe Ni dhambi ya Kutoka kwa WAGANGA mikataba Yao walikuaganisha uendelee kuwa chini ya utumwa kwa jina la Yesu Leo Utoke nje Toka nje ya agano lao Toka nje ya utumwa wa mapepo Inuka na Simama Hakuna nguvu itakayokuagusha katika jina la Yesu;
Amen

Naitwa Bishop Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768
Kanisa Huduma ya ROHO MTAKATIFU (Holy Spirit Ministry Tanzania)
Fb;Moto wa Yesu

KUINUKA NI NINi?
Ni Hali ya Mtu kusimama imara bila kuyumbishwa yumbishwa na elimu za Shetani au za kipepo au nje ya Mungu.

LENGO KUU LA SOMO LETU;
Tunapaswa Kusimama imara dhambi na Elimu ya Shetani isitutawale akilini mwetu Tusimpe Sifa na Kumtukuza Shetani hata Kama  Tutapita Wakati Mgumu kiasi ngani inapaswa Tumtukuze Mungu tu.

WALENGWA; Waliokoka na Wenye Imani na Mungu njisi zote.
Umri 18-80

FAIDA ZAKE UNAPOINUKA.

1:Utasimama hutaanguka
2;Utavuka magumu
3;Utaielewa elimu ya Kiungu Shetani hatakug,oa
4:Utashuhudia na Kumwinua Mungu hata katika mapito
5;Utakihesabu Kila ulichotendewa Ni Mungu ametenda.
Nk

HASARA ZAKE USIPOINUKA
1:Utaanguka Kila ufanyacho hakitasimama utakavyo.
2:Hutavuka vipindi vigumu utazidiwa na kelele za Shetani na
Maneno Yao.
3;Utamtii na kumsikiliza Shetani katika wazo lake na Elimu zake.
4;Hutashuhudia Bali Utaendelea Kupingwa na majira.
5;Utainamania na kuyatukuza mapito hutajipa matumaini.

YUPO MUNGU
Sauti yake Inakuita inakuambia Inuka Inuka AMKA AMKA SIMAMA SIMAMA

MUNGU ASEMA KWAMBA
Najua Yu DHAIFU lakini kwa nguvu zako hizo chache Utamwangusha Adui Yako Simama na Inuka kwa Hasira ya Wokovu

Nimekuita Utoke Katika shimo la watesekao Ukawe huru.

Ni Mjumbe Mwaminifu Wa BWana Pastor Richard
Ninakuambia INUKA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.