SOMO; CHAZO NI NGUVU CHACHE

✍🏾✍🏾🔥🔥SOMO; CHAZO NI NGUVU YA ROHONI SIO YA MWILINI🔥👏🏽👏🏽

Shalom Mwanangu Karibu Katika SOMO LA LEO CHAZO CHA KUSHINDWA NA ADUI NI NGUVU ZA KIROHO KUWA CHINI

Tufunue Biblia Zetu Tusome Vitabu hivi; 1Timotheo;4;8 Marko:1;43, 3;27, 5;4 Warumi;4;20 1Wakoritho;1;27 Zaburi;18;1-39 Kutoka;1;20 Waefeso;4;13
                            ✍🏾✍🏾🔥🔥 UTANGULIZI🔥👏🏽👏🏽

Karibu Leo Tujiulize Kwanini Tunazidi Kupingwa Kiroho hatukui kiroho bado Shetani ameendelea Kututumikisha na kila kukicha Tunatamani Tutoke Kwenye Mateso haya lakini Tunaishia Kujipa moyo Bado Tunazidi Kuelemewa na inaonekana hata mbinu anayoitumia Shetani bado Kwetu Kama watoto wa Mungu inatupa shida njisi ya ustad wake na umahili wake wakututandika Bado unanguvu Kwa Sababu ngani Shetani Anazidi kutupatia magonjwa kutupatia Mateso minyororo mpaka imefikia Kumshusha uwezo wa utendaji wake wa kazi na Kuaza Kusifu nakutukuza matatizo yetu bila kujua Tunainua Utukufu wa Shetani.

Kumbe Tumepingwa sababu nguvu Zetu Ni chache kiroho nguvu chache za kuhimili mikiki ya Vita vya kiroho wengi Tunaitazama Vita ya Kiroho Kama Vita ya Maji maji na mwisho wa siku Tunapingwa Sisi watoto wa Mungu au Tunazidiwa Tunaanza Kukata Tamaa Tunarudi nyuma kiroho na Kuanza masononeko Mungu ooh Umeniacha Mungu mbona hujibu

Neno Linasema ufalme wa Mungu na Baraka Hutekwa na wenye nguvu mtu mwenye nguvu huwa Hashindwi kizembe anapambana Kufight mfano; Kama steringi wa mchezo au Tamthilia wewe Ni steringi ili ukamilike kuitwa steringi Lazima umshinde Shetani hata Kama Amekutandika hutamani hata kuomba lakini Uelewe wewe mshindi.
Mathayo : Mlango 11

12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Bado Biblia inasema Mtu mwenye nguvu huweza kuingia kwenye nyumba ya Mtu aliyedhaifu na Mtu mwenye fikira za kumtazamia Mungu wake uwezo wake mdogo kuliko Tatizo alilonalo

Mathayo : Mlango 12

29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake

Nimeabatanisha hii Mistari uelewe kwanini Yesu Alitolea mifano hii 

Karibuni Naitwa Pastor Richard Ndiye ninayekuwasilishia SOMO Hili Kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu


Lengo Kuu la SOMO; Tuwe na Nguvu za Kiroho na sio MWILINI TU

Walengwa WA SOMO; miaka 10-50 wanawake na wanaume Linawalenga

Simu ya kuongea na Bishop Richard+255759861768 Jioni Mpigie

Makao makuu Morogoro veta Dakawa

Kanisa la Holy Spirit Ministry Tanzania

Kuna AINA MBILI ZA NGUVU KWA MTU.

1:Nguvu ya ROHONI
2:Nguvu ya MWILINI

NGUVU YA MWILINI;(1timotheo;4;8)
Hii huwa nguvu anayokuwa nayo mtu ya kuulinda  mwili wake na kujilinda mwenyewe Kimwili TU lakini Kiroho anakuwa Hana nguvu ROHONI.

Faida ya hii nguvu
1;Hukuepusha na magonjwa nyemelezi
2:Huufanya mwili wako uwe imara
3:Hufanya akili na mawazo yaweze kufanya kazi 
4;Hukupa nguvu ya kujitetea na maadui wa MWILINI
5:Hufanya mishipa na mfumo wa Damu uweze kufanya kazi kwa usahihi.
6;Hukuepusha na Presha moyo nk


HASARA ZAKE USIPOKUWA NA NGUVU YA MWILINI.

1:Utapata magonjwa Kama moyo kutanuka presha unene usio na faida mwili wako kuumwa umwa nk

2:Mwili wako Utakuwa dhaifu na Lengevu.

3;Akili na mawazo Yako itashindwa kutatua changamoto zako

4:Damu na mfumo wa mwili huwezi kufanya kazi sawasawa


Unashauriwa Fanya Mazoezi na Utakuwa na nguvu ya mwili Tembea kimbia ruka kamba Fanya mwili wako uwe na Afya.

Kuna watu wanateseka matatizo yao yanaitaji TU mazoezi Ili uweze kushinda na Kutoka kwenye mikono ya Magonjwa au presha

NGUVU YA ROHONI

Hi huwa Ni nguvu ya Kiroho inayojumuisha Mambo matatu ndani ya Mtu

1;Uwezo wa Kukabiliana na Kitu Kiroho

2:Imani ya Kukabiliana na Kitu Kiroho

3:Roho ya Kukabiliana na Kitu Kiroho

UWEZO WA KUKABILIANA NA KITU KIROHO

Ni Mtu kuweza Kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi KIROHO

IMANI YA KUKABILIANA NA KITU

Ni Mtu kuweza kuwa na nguvu ya kuzidi Imani ya Kile anachokabiliana nacho kuazia kiufahamu kiuelewa Kifikira Anavyotamka vinamdhihirishia yeye Hashindwi Kitu hapokei matukufu ya Shetani au kukiri kushindwa mtazamo wake upo juu

ROHO YA KUKABILIANA NA KITU KIROHO

Tunamanisha Uwe na nguvu ya Kumjua ROHO MTAKATIFU katika Majukumu Yake ya wewe Kukusaidia na njisi ya kumtumia kwa Usahihi hapa huhitajika ufundishwe Kazi za ROHO MTAKATIFU ndani yako na ndio maana mnaokuja kanisani hapa nawafundisha Neno la Mungu na mnafunguliwa katika Neno la Mungu Bila Neno la Mungu huwezi kushida

VITU NGANI VINAKUPATIA USHINDI KATIKA VITA VYAKO VYA KIROHO.

1; Mafundisho ya Neno la Mungu Yenye uhai wa Uvuvio wa ROHO Mtakatifu.

2;Maombi 

3:Sifa na Kuabudu

4:Uaminifu Wa Zaka na Michango

5:Ibada na Mungu.


Shika Sana Mafundisho na Maombi Utavuka mapito yako

VITU NGANI UEPUKANE NAVYO VINAVYOWEZA KUKUFANYA UENDELEE KUSHINDWA

1:Mafundisho yasiyo na uhai.

2:Makundi Makundi

3;Kukaa na Waliokata Tamaa au Kushauriana na aliyekata Tamaa

4:Watu wanaokushauri na Kukushawishi uende kwa WAGANGA 

5;Kuamini Umeshindwa au Kulipa nguvu Tatizo.

Epukana na Haya ili Ushinde Uwe na nguvu ya kushinda


FAIDA ZAKE UNAPOKUWA UNANGUVU YA KIROHO

1;Utamshinda Shetani na majeshi Yake

2;Unafanikiwa kiroho na kimwili

3:Utaangusha ngome nyingi na utamiliki vitu.

HASARA

1:Kuwa Mtumwa wa Shetani na falme zake

2;Unashindwa kufanikiwa kiroho na kimwili Unashindwa

3;Utaangushwa na kuonewa Sana


HITIMISHO AU WITO WANGU

Tupende Neno la Mungu Mafundisho yanayotuinua kiroho na kutumwangilia vyema ambayo yanatupa kukua kiroho sio Tupende Mafundisho TU kulingana na mapito yetu tu


Basi Kila MMOJA Tukaombe Pamoja Mungu Atupe mwisho wenye nguvu vizuri

Baba Tunakuomba Wanao Uendelee kutujenga Katika nguvu zako Katika uwezo wako uweke ndani yetu mamlaka yako Yenye nguvu na Utawala Tukaangushe Kila fikira na wazo la kututazamisha kushindwa katika jina la Yesu;

Amen:

Naitwa Bishop Richard

Nipo Morogoro Veta Dakawa

Simu+255759861768 jioni kupiga


Mbarikiwe Endelea kushare kwa wengine






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.