Somo; Nimechoka
🌳🌳SOMO: Nimechoka Na Matatizo Yasiyoisha🌲🌲Mungu wangu usiniinulie Kisasi mwanao Niokoe Na Mateso haya🌲🌲🌳
Vitabu;Zaburi:6;6 Zaburi:69:3 Yeremia;6;11 Yeremia:45:3
Ayubu;10;1-5
Inafikia hatua Tunapoona Mambo yanazidi kuharibika na kuwa magumu Tunaamua kikri Nimechoka na majaribu haya hata Kama ndio Mungu umeamua kupima Imani yangu sio kila Siku Mimi Tu Nimeomba Sana Lakini Naona Kama Umefumba masikio usinisikie Huwa Tunaenda mbali mpaka Tunaacha kwenda Kanisani nakuwachukia WATUMISHI au Wanaotendewa Kwa Sababu ngani Tumechoka na Teso Hilo.
Je Kwani Wewe Ukinuna nakuchukia Usipite kwenye pito Unaweza kumfanya Mungu Akuhurumie asikupitishe kwenye Jaribu linaloenda kukupa sifa ya Kumtengemea
Je Ukiacha Kwenda kanisani Nakuomba ndio suruhisho ya Tatizo lako Unakuwà unamkomoa Mungu au mwenyewe
Je ukisema Unaanza Kurudi nyuma Unaacha Wokovu harafu mchungaji wako akikuuliza unamdanganya unazani ndio Utavuka kwenye pito
La hasha!!! usijidaganye kumuacha Mungu au kuwachukia Wachungaji wako kisa unapitia pito mbali Simama katika Nguvu ya imani Utavuka Pito lako Jaribu harikimbiwi Siku Zote hushindwa kwa Uvumilivu Tu.
Jaribu la ndoa Yako Jaribu la Afya Jaribu la Uchumi Jaribu la Uzazi Acha kurudi nyuma au Kumuacha Mungu au kuwachukia WATUMISHI kisa umeombewa Sana hujajibiwa.
LENGO KUU LA SOMO; Tuvumilie Majaribu Yetu Maana ndio Mtaji wetu wa Imani ya kweli;
FAIDA YA KUENDELEA NA MUNGU HATA KAMA MAJIBU YAMECHELEWA.
1;Huwa Lazima Imani Yako inakuwa na nguvu yakuhamisha Matatizo.
2;Huwa Unakuwà jasiri Kumtengemea Mungu sio Mwanadamu
3:Unajua kuomba hata Kama Ni mvivu Utajua na kufunga kabisa si mchezo.
4;Imani yako Unakuwà wa kuwafariji wengine wanaokata tamaa.
5;Unayaona majibu Zaidi ya ulivyomwambia Mungu atende Yaani hujibiwa mfululizo ndoa Mtoto kazi zinafatana tu.
6;Huwa shahidi wa kweli wa Imani ya Kikristo
7;Utaona Mungu Anajibu Mengine Yote lakini Ambalo ametaka akufundishie Imani yako hutajibiwa hata dalili tu hutaona ili unune vizuri na uaze kunug.unika vizuri.
HASARA JAMANI ZA KUANZA KuRudi NYUMA AU KUNUNA NA KUCHUKIA SHUHUDA ZA WENGINE UNAKUTA MTU ANAHAMA NA KANISA.
1;Kukata Tamaa na Kutokujibiwa kabisa
2; Uvumilivu huisha na mtu anaanza kuwasema vibaya Wachungaji. Ooh Pastor Richard Kaniombea Mimi sijajibiwa ooh Shuhuda za Uogo Kanisa lile mchungaji wake hajui kuomba nk
3;Mtu huiacha Imani ya Kikristo nakuanza kwenda kwa waganga wapinga Kristo kusomewa nyota nk
4:Mtu huanza Kukri kuwa Labda Mungu Mimi Ameniandikia nisiolewe labda Pastor Richard Mungu Ameniandikia nife na ugonjwa huu no
Ukimkuta mtu anaanza Kukri hivyo ujue Ameshachoka na Jaribu Tu imani Yake CHACHE.
5;Huwa Anajiona Kama watu wanamdharau au kumcheka kumbe sio Ni fikra zake TU Watu wanamheshimu.
6;Huwa Mtu anazidi kujifunga anafikiri Mungu Ni Wa rushwa Utaona Pastor Mungu akinipa Mtoto nitajenga Kanisa halafu akijibiwa unazani Tena Utamuona Kumbe alitamka TU kwa kuwa alikuwa Amechoshwa na matatizo
UNATAKIWA UJUE UFALME WA MUNGU HAVIINGII VINYOGE HAVIINGII WANAOKATA TAMAA KUUTAFUTA USO MUNGU HAINGII Mwenye KUNUNA Na KUCHUKIA IBADA
Biblia inasema Furahini Tena nasema Furahini katika Bwana
Wewe kwanini Unanu na Unapanga mpaka uiche Imani yako.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro-Tanzania
Simu+255759861768 WhatsApp nifate.
Maoni
Chapisha Maoni