SOmo ;Mungu Akuheshimishe
⌚⌚SOMO; MUNGU ANAIRUDISHA HESHIMA YAKO WALIOKUDHARAU ANAWAFUNGA VINYWA VYAO⌚🗣🗣🗣
Nahumu;2;1-13 Yohana;4;44 Mathayo:13:57 1coritho:12;21-25
Waebrania:2;7-10
Wahenga walishasema Usimdharau mtu kabla hajafa huwezi ukajua atakuja kuwa Nani Heshima na Thamani ya Mtu ipo katika uhai Wake TU maana unayemdharau Leo kesho hujui utamkuta wapi
Karibu Naitwa Pastor Richard Kwa Wageni Ambao ndio mmeanza kunifatilia Kurasa na group Zangu Nipo Morogoro Veta Dakawa nchini Tanzania
Lengo Kuu LA SOMO Hili; Tujifunze kuwaheshimu wakubwa kwa wadogo Usimdharau mtu hata Kama kaja ofsini kwako Jitaidi kumkalimu na kumfundisha au kumhudumia vyema ili hata siku nyingine akukumbuke Usiwe na majibu machafu au kuwadharau wengine waheshimu wote.
Nini Maana Kudharau Ni Hali ya kukiona kitu hakina thamani hakina umhimu kwako Tena.
Tambua kila mtu Mungu amemuweka kwa kusundi maalumu mpango mwalimu usiaze kuhesabu madhaifu kwa mtu ukakosa kukumbuka ipo siku madhaifu yataonekana kwako
Heshimu mtu ili upate kuheshimiwa na Mungu hata mbingu ikutambue ifunguke ikubariki
Lakini kwa kuwa umekuwa mtu wa Kudharau wegine hata Mungu amekudharau fahari yako haionekani Tena
Mbigu zimekudharau Baadala ziachilie majibu kwako zimeachilia mateso kwa Sababu ya dharau tu
Unawaona wanadamu wezako Kama Hawana maana Yoyote Yamkini umejariwa kidogo tu upako na uchumi lakini Baadala uende juu Umeanza Kushuka chini kwa kuwa mbigu hazikutambui Tena
Mungu anaamua amwinue yule uliyemdharau nakumpandisha cheo ofsini kwa kuwa mlikuwa mnamdharau halafu uliyekuwa bossy wake umeshushwa cheo
TuTAPONAJE
1;JIFUNZE kuheshimu watu wote
2;Usijione Acha watu wakuone wao
3:Usipende Ushirikina mpende Mungu
4;Wapokee wachungaji na maskini nyumbani kwako upate Baraka
5;Usiwaseme watu au kuwanyima chakula walishe Wageni washimbe
6:Usiwe na Tabia ya kuonesha unawakarimu watu wakitoka unaanza kuwasema vibaya.
7;Nenda ibadani na penda Neno la Mungu
8:Wasaidie wasiojiweza hasa walemavu wajane yatima
9;Watete wanyoge wapate haki zao
10;Fanya haki usibangue mtu au kupendelea
Tukifanya haya Mbigu zitafunguka nakumwanga Baraka mpaka Tukimbie
Naitwa Pastor Richard
Maoni
Chapisha Maoni