SOMO:NJEGA Misingi YAKO ILIYOHARIBIWA NA UFALME wa NGIZA
✍🏾✍🏾SOMO;HARIBU MISINGI MAADUI ZAKO YOTE✍🏾✍🏾✍🏾
Vitabu;Mathayo:7:25 Luka:6;45 Matendo:16:26 Waebrania;4;3 Isaya;54;11
Karibuni Katika SoMo Hili Wanangu Naitwa Pastor Richard SoMo Hili nikiwa Nakuletea
Lengo kuu la SoMo; Kufichua ufalme wa ngiza ulioharibu Misingi yako Iliyojenga Mateso Kupitia Misingi mibovu na Kujenga Msingi imara uliosimama imara.
Misingi Ni Nini?
Ni Kile kinachoshikilia ukuta au kusimamisha nyumba Nzima hiyo kimwili lakini Kiroho ni kitu kinachoshikilia imani yako na kukujengea udhaifu wa Kuamini uweza wa Mungu pia Misingi Ni Tabia inayoweza kuendesha maisha yako nakukuongoza kutatua kitu.
Katika Uharibifu majeshi ya mapepo na wachawi hujenga Misingi Yake pale yanapoingia ili kuufanya mwili wako uwe Na Tatizo
Hujenga Misingi ya Hofu woga ambayo Hufanya uhabifu wa maisha yako kwa ujumla
Hujenga magonjwa mateso nk ambayo huwa misingi ya uharibifu wa Afya yako chazo Ni majeshi au Tabia
Hujenga Misingi mibovu ya Tabia yako yenye kukuendesha nakukufanya ushindwe katika Jambo au uogope
Kwa ufupi chazo Cha wewe kukua kiroho au Kushuka kiroho Ni misingi unayokuwa unajengwa ukiokoka Misingi ukiokoka ukajengewa Kuamini kuwa H.I.V haipone ujue huo Msingi Utaendeleaa kukutesa Msingi ukijengewa kuwa usiwe unaomba hata ukikua Utaendeleaa hivyo Msingi Kama ukijengewa Kuongozwa na Kuzidiwa matatizo hivyo hivyo hutakuwa na nguvu yakutoka kwenye Tatizo.
Misingi yako ikiharibiwa ndio dira nzima ya maisha yako imeharibika
Biblia inasema
Zaburi : Mlango 11
3 Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?
Ni swali la kujiuliza Misingi yako ikiharibiwa unatakiwa Ufanye Nini ?
Jibu: Misingi ikiharibika inatakiwa nyumba nzima ibomolewe ianze upya kujengwa ndivyo hivyo hivyo mtu aliyeupokea wokovu ikiwa alijengwa kuona Kuna magonjwa ambayo Mungu anayaponya na mengine haponyi Kuna Mambo ambayo Mungu anayaweza na megine hawezi lazima Yule mtu Aanze kujengwa upya katika Imani Yake ibomolewe ile ya kuona Tatizo linauwezo Mkubwa kuliko Mungu.
Zaburi : Mlango 104
5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake,Isitikisike milele
Pia ikiwa Biblia inasema aliweka Misingi Yake toka dunia ilipoumbwa ujue hata wanaomwamini Anawajenga katika Misingi mikubwa Sana ya Imani
Isaya : Mlango 40
21 Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia
Tunapaswa Kujua Kitu Kila Kitu Kisipojengwa katika Misingi imara huwa kinaharibiwa na muovu
Ezekieli : Mlango 13
14 Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA
Kumbe ili tujue Yupo Mungu Ni Lazima Iharibiwe Misingi nakubomoa kila Misingi mibovu ambayo Shetani na ufalme wa ngiza.
Tunaona katika Nguvu iliyokuwa imewatesa Paulo na Sira ili wafunguliwe ilibidi Misingi ibomolewe Tunaona hata Yesu alipoamua kuleta wokovu lakini Ilimlazimu kubomoa Misingi yake ile aliyoikuta nakuujenga ufalme upya na Misingi upya nasi Tunatembea ndani ya Misingi Yake.
Matendo : Mlango 16
26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
Luka : Mlango 6
45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.Misingi Miwili
Faida Ya Wewe Kuharibu Misingi.____Kujenga misingi ya Kiungu
1; wachawi unawafanya mitengo Yao isikunase
2;Unaponywa vitu vingi kwa wakati mmoja.
3:Imani yako inajengeka kushinda Vita
4:Hutakuwa na Mashaka na utendaji wa Mkono wa Bwana.
5: Utafunguliwa Minyororo iliyounganishwa na Tabia yako.
6:Maisha yako na Matendo yako yatabadilika
7:Milango iliyofungwa kwa Siri itakuwa wazi
8:Baraka za Uzao Baraka za mazao Baraka za afya nk zitakufata
9:Watu watashuhudia kuinuliwa na Kubadishwa kwako
10;Mambo yako yataanza upya katika Ushuhuda wa Ushindi
HASARA za KuTokuharibu Misingi ya Shetani hii
1: Wachawi watakunasa katika mitengo Yao
2;Hauponywi vitu vingi kwa wakati
3:Imani yako inajengeka kushindwa Vita na Kupingwa kiroho
4:Utakuwa Mtu wa Mashaka na Utendaji Mungu Utaona Megine hayawezekani
5;Hutafunguliwa au Tabia kubadilika itaendelea ile ile hata kabla hujaokoka.
6;Maisha yako hayatabadilika chochote kiroho na kimwili
7; Utaendeleaa kuteswa kwa Siri na kufungwa Ufahamu na majeshi ya ufalme wa ngiza
8:Utakuwa na Laana na Magonjwa wewe na Uzao wako watapingwa
9;Watu watakuona palepale wengine wanamvu wewe Upo Hali hiyo hiyo
10:Mambo yako yataanza kuharibika Kushuka chini kila kitu.
Nini Ufanye Sasa Kama Unataka Ujenge Misingi upya
1;Okoka na ubadilike ufate wokovu so Dhehebu
2;Tafuta Mlezi wa Kiroho atakulea kukuongoza na kukushauri hiyo
3;Simama katika uaminifu kila mwenzi kutoa Fungu la kumi kwa Baba yako Mlezi wa kiroho katika Madhabahu yako usikubali kuacha au kutoa katika eneo lisilo lako
4;Fundishwa Neno na Upende Kujifunza Neno la Mungu
5;Usikubali uaze kulipa madeni ya kimwili kabla ya Deni la Fungu la kumi Kama unadaiwa
Malaki:3:10
6:Usimwongope Baba yako wa Kiroho kumweleza Kile kinachokuzuia na saa nyigine nenda kanisani kafanye kazi za kanisani tu
7:Anza Kujifunza Kuomba kidongo kidongo Utajua kuomba vizuri
8:Tenga muda wa Kuomba au Kupitia mahubiri mbalimbali ya Wachungaji mtandaoni kwenye Vitabu nk
9;Wazoeshe wanao kwenda kanisani na kuomba
Mithali:3:1-6
10:Wajengee watu Wegine Imani ya kuwa Mungu Yupo anatatua matatizo Haijarishi Liwe umepitia muda ngani walete watu Wegine kanisani wakutanishe na Baba yako wa Kiroho ili nao wasaindiwe
Nakutakia Baraka za Kufunguliwa kila sehemu Mwanangu Namtuma MALAIKA atangaze Vita kwa walioshika maisha yako awapinge wote MALAIKA asimame kwenye malango Yao katika jina la Yesu;Amen
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Simu+255759861768
Maoni
Chapisha Maoni