SOMO :HIZI NDIO NJIA UTAMJUA MWANAUME TAPELI WA MPENZI MHARIBIFU
SOMO: HIZI NDIO NJIA ZA KUMJUA MWANAUME ATAKAYEKUOA USIPOPATA SIFA HIZI UJUE HAMUOANI
Bwana YESU Asiwe watoto wa MUNGU
Haya masomo nayaleta kwa Vijana wote wakae wajue na kuepuka kupitia katika4 Machungu YA kusalitiwa katika Mapenzi
Kwa sababu vijana wengi siku hizi hutumia njia ya kusema kuowa wakiwa wanataka Bint wampate wazini nae tu kisha wamzalishe au kumharibia malengo yake na mipango.
Binti Yangu nimekuletea Somo hili Ambaye hujaolewa Ujue sifa ya mwanaume muoaji Anakuaje Hii ikupe ufahamu. Usijirahisishe na kukubali kuitwa mama kabla ya kuitwa mke wa mtu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
nakuandalia nakala hii fupi yenye maarifa makubwa.
Tunasoma Zaburi 119:9
Mithali 7:7
1.MWANAUME MWENYE LENGO LA KUKUOA ATAKUPA NAFASI YA KWANZA KWENYE MAISHA YAKE.
Yaani ktk mahusiano ya uchumba tu utaanza kujiona queen. Wanaume waoaji tunafanya hivi ili ndege mzuri asirukie mti mwingine kwa hiyo baada ya ndoa mambo yakibadilika usishangae sana ni kipindi cha mpito tu upendo unakuwepo pale pale isipokuwa wengi wanajisahau kwa sababu wameshapata. Mwanaume ambaye wewe sio namba moja wake ujue hana uhakika kama atakuoa. Kwa mfano kama mawasiliano yenu ya kubeep ujue anakupotezea muda. Mwanaume ktk uchumba hata kama yuko bize kama maji ya mto hawezi kukosa nafasi, muda au mb za kuchat na ampendaye.
Niwape angalizo wanawake: Ukiona unatumia nguvu kubwa kumshawishi mwanaume akuoe na kama katika hatua za uchumba tu mambo mengi anafanya bila kujali utasema nini au utajisikiaje ujue unalazimisha kubeba gunia la misumari. Jiongeze mapema!
2.URASMISHAJI WA MAHUSIANO.
Mwanaume anayetaka kukuoa ataweka rasmi uhusiano wenu kwa wazazi na viongozi wa kidini. Lakini sio lazima afanye hivo mapema bali atajipa muda kidogo wa kujiriddhisha, cha msingi ni kuangalia na vigezo vingine kwanza maana kurasmisha huku ni hatua kubwa ya kukaribia ndoa so haifai kufanya kwa haraka.
3.MWANAUME MWOAJI HAPOTEZI MIAKA MINGI KWENYE UCHUMBA.
Kwa asilimia kubwa ukiona miaka 4,5..nakuendelea .. Kila mwaka anasema anajipanga lazima ujue huyo sio mwoaji. Wapo wachache wanaofanikiwa kukaa uchumba miaka mingi na kuoa lakini katikati ya miaka hiyo kuna maumivu yasiyo ya lazima, kuzalishwa kabla ya ndoa au pengine alikuwa anatafuta mtu mwingine alivomkosa akaamua aoe yule yule aliyenaye.
4.MWANAUME MWOAJI ANAJIPANGA KIMAISHA.
Mwanaume mwoaji utaona anavyohangaika kuweka mambo yake sawa kiroho na kimwili maana anajiandaa kuanza kubeba majukum. Hapo utaona anapunguza matumizi yasiyo ya lazima, anapunguza marafiki wasio na tija. Na katika mipango yake mingi atakushirikisha ili akushawishi indirectly uone kwamba ukiolewa naye huwezi kuwa na maisha magum.
5.MWANAUME MWOAJI HANA HARAKA NA PENZI LAKO.
Wanaume wengi wanaodai penzi kabla ya ndoa lengo lao ni kuonja na kuacha. Watu wa aina hii ukiwazuilia usishangae kusikia ameanza mahusiano na mwanamke mwingine. Isikupe shida kwa sababu hakuwa na upendo wa kweli kwako.
6.MWANAUME MWOAJI ANA SHAUKU NA WEWE.
Kwa kuwa anakupenda kweli na anataka kukuoa utaona bila hata kujipanga kwa maneno yake utagundua anatamani kuishi na wewe. Haachi kuifikiria arusi yenu itakavyokuwa. Haachi kufikiria honeymoon yenu mtaspend wapi. Haachi kufikiria mipango yenu baada ya honeymoon. Haachi kuleta vizawadi vya hapa na pale. Hawezi kuficha shauku yake ya kutaka kuishi na wewe mapema iwezekanavyo maana anahisi akizubaa kuna mtu mwingine atakuja kukuoa. Na kwa kweli ushauri wangu kwa wanawake ukiwa kwenye uchumba usio na dira mtu anasema anakupenda lakini hajui atakuoa lini then akaja mtu serious anataka ndoa mchunguze miezi angalau 6 nenda kwenye uchumba angalau mwaka mmoja kisha olewa tu.
7.MWANAUME MWOAJI AMEJAA MSAMAHA.
Ukiwa na mwanaume kwenye uchumba kila kitu anakuadhibu. Mara matusi, hujakaa sawa ngumi, au kosa dogo amekublock wiki zima unatoa machozi ohoo ujue sio mwoaji huyo bado anacheza na ujana ndio maana hajali hisia zako. Mwanaume mwoaji ni mwelewa, kuna wakati anakosoa na kukasirika ili kukuonesha hapendi ujinga lakini sio ile too much. Mwanaume mwoaji ana staha na moyo wa msamaha coz hata yeye hatamani kukupoteza. Ila kama hana mpango na wewe ohoo utajionea mwenyewe jinsi gani hashtuki. Na muda wowote ule anasema "kama unaona huwezi kufanya kile nasema tafadhali tafuta mwanaume wa kukufaa"
🔴 Ukiambiwa hivo mara 3 ujue hakuna ndoa kama ipo unalazimisha na utavuna unachopanda. Ni ishu ya kuelewa lugha na saikolojia tu.
8. *MWANAUME MWOAJI NI MFUATILIAJI* .
"Akikwambia utoe taarifa kwamba anataka kuleta posa kwenu atakufuatilia kujua kama umefanya hivyo. " Ukimshirikisha mambo ya kazini kwako au biashara zako au kanisani kwako baadaye atakuuliza ajue unaendeleaje coz tayari anajiandaa kuwa kichwa chako. Ukiona una mwanaume hajui unaendeleaje na mambo yako ujue bado hajakomaa hata kama akikuoa kwa wakati huo hatajua umhimu wako ndani.
9:MWANAUME MUOJI Anahofu Ya Mungu
Kwa kuwa anakupenda hatataka ukakwanze au kukusaliti anakuwa na hofu ya Mungu.
10:MWANAUME MUOAJI NI MUELEWA
Mwanaume muoaji huwa chochote ukimwambia anaelewa hapendi ugomvi au ukimwambia tuachane Anaelewa hataanza kukutukana au kukufanyia vituko Ni mtu asiyependa makuu Lakini ukikutana na mwanaume ambaye siyo muoaji ataanza kukutukana nakudai vitu alivyokupatia mkiwa na kwenye urafiki.
Naitwa PASTOR RICHARD
Nipo Morogoro VETA
WhatsApp +255759861768
Tovoti www.mchungajirichardi.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni