SOMO; MALAIKA WANAVYOKUPELEKEA OMBI LAKO

✍️SOMO: MALAIKA WANAVYOKUPELEKEA OMBI LA HITAJI LAKO KWA MUNGU

Tufunue; Vitabu hivi
Zakaria:1;4-10,5;5,Mwanzo:22;15,Waebrania:2;5-7,Luka:1;11 Maamuzi;13:15-20

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Karibu Katika Kipindi Cha Neno la Mungu.

Leo Nataka Niongelee Na Kufundisha Juu Ya Malaika walinzi ambao pia huwa wanabeba dhamana Yako ya kuchukua Maombi Yako pale unapoomba Huchukua Yale Maombi Yako nakuyapeleka mbinguni.

Maombi Yako Kama Malaika wako Anayebeba Maombi Yako Kuyapeleka Kwa Mbinguni hatayafikisha Ni ngumu Mungu Kukujibu

Tuchukue Mifsno Kadhaa kwenye Biblia.
Tunaangalia mzee wetu Ibrahimu Alitengemea Apate Mtoto bado kijana Akaja Kupata akiwa na Miaka 99 na mkewe 80 Lakini Ibrahimu alimpenda Mungu na Alikuwa mtoaji wa Zaka kanisani Alimtumikia Mungu lakini Alikuwa Akiomba Mungu nipe Mtoto asipokee. Kwa Sababu ngani Maombi yake hayakumfikia Mungu mbinguni Kutokana na Malaika wake Aliyekuwa Amebeba Maombi kuzuiliwa Angani na Kadiri alivyozidi kuomba aliyapa nguvu Maombi yake yapite Vizuizi mwaka 20 Ndio Mungu Anakuja Kumjibu kumpa Mtoto Alitulia Nakuomba.
Mwanzo:22;15

Mfano mwingine
Daniel Tunaona kwenye Biblia Alitupwa kwenye tundu la Simba Alitengemea Ataliwa na Simba Wenye njaa Malaika Mlizi Akawafunga vinywa wasimdhuru Biblia inasema kwa Sababu alikuwa anaomba Maombi Yake Danieli hayafiki mbele za Mungu Malaika Alizuiliwa mkuu wa Anga.

MALAIKA ANAPOYACHUKUA MAOMBI YAKO KUYAPELEKA MBINGUNI.

Mungu aliweka utaratibu huu wa kuwa unapoomba Mahitaji Yako Malaika waliotengwa kwa Ajili ya kukusanya Mahitaji ya watu wanayachukua na wanapoyachukua Maombi Yako huyapeleka Moja kwa Moja mbinguni Malaika yule akifika kule harusiwi kumpelekea Mungu Mahitaji Ampe Kuna Sehemu Kama chetezo fulani Anafungua Anaweka Kila Siku hukusanywa pale Maombi ya wanaomuomba Mungu.

Kwenye Utukufu wake Mungu pale Wapo Makerubi Kerubi kule mbinguni Ni Malaika wenye cheo kikubwa kuliko wengine na huwa Wapo wamemzunguka Mungu Wakimwambia TU wastahili Bwana Wastahili Wastahili Kupewa Sifa Wastahili Kuongopwa wewe(WANAMTUKUZA Mungu) Mungu huteua mmoja kila Siku Kwenda kuchukua Yale Maombi yaliyomfikia hapo Kerubi humpa Mungu na Mungu hujibu Maombi Yale hapo papo humfikia Mlengwa Pale akiweka sahihi yake ameyapokea huku unauona mkono.

CHANGAMOTO
Ni Malaika Mpaka ayafikishe Kule huwa Kuna Vita na Vizuizi anavyovituma Shetani kuyazuia Maombi Yako kwa kupambana nae.

Vita huazia Anga la Kata,wilaya,mkoa,Nchi,Bara,Dunia,Lusifa mwenyewe Sasa Akiwapinga nakuwashinda hukutana na Shetani Anamzuia Maombi Yako yasifike

Tambua Malaika Ni roho Hawana mwili wa Uharibifu Kama wetu wao mwili wao hawafi hawaoi hawazeeki.

Mkuu wa Anga Ni Jini Anayeratibu shughuli za kupiga Maombi ya watakatifu waliopo duniani nayo huwa Ni roho

Ikitokea Malaika wako Amedhibitiwa na Hizi roho hutaona majibu utajipa moyo Maombi Yako Mungu Ameyapata kumbe hayajamfikia na wewe Wala huombi na Wala Kuombea Maombi Yako yawe na nguvu utajikuta umebaki kwenye Tatizo hivyo hivyo

HAKUNA UTARATIBU WA MUNGU KUPOKEA OMBI LAKO BILA HATUA AU UKAENDA MOJA KWA MOJA

MALAIKA Ni watumishi Mungu watenda kazi wa Mungu kule Mbinguni Baba Mwana Roho Mtakatifu Ni watenda Kazi wanaohidhinisha na Waamuzi wa mwisho kule mbinguni na Duniani

Mungu kapangilia utaratibu KILA kundi la Malaika na majukumu Yake yanayohusiana na Mwanadamu kuhakikisha Mwanadamu Anatembea katika utaratibu wa kujua Yupo Mungu

Mhimu Sana unapoomba Kuombea Maombi Yako.

✍️✍️Mambo yanayomfanya Maombi yafike.
1;Kumtumikia Mungu kwa Mali zako
Kuwa Mwaminifu kutoa Fungu la kumi kila Mwenzi
Ni Sheria hiyo kwa Mungu.
2;Imani na Ukomavu wa Akili kupanda kwa kiwango Cha Kumjua.

3;Kiri jina la Yesu na Utawaliwe na Hofu ya Jina lake.

4;Mwabudu Mungu Msifu Omba Na Kuwa Na Muda kila siku na Mungu

5;Yatie nguvu Maombi Yako yafunike na ulizi muombee Malaika Wako Vizuizi avuke. Asizidiwe.

NINI UFANYE KAMA MAOMBI YAMECHELEWA KUJIBIWA

1;Kuwa Mwaminifu kwa Mungu kila Mwenzi toa Fungu la kumi linenee Mahitaji matatu magumu yaliyoshindikana.

2:Tenga Muda wa Kuomba Na Usiache ibada nae.

3;Muombee Malaika wako Anayebeba Maombi Yako.

FAIDA NGANI UTAZIPATA UKIFANYA HAYA MATATU.
1:UTAJIBIWA
2;Milango itafunguka
3:Utaona wepesi Mambo Yako
4;Utaona mabadiliko katika Maombi Yako
5; Madhabahu iliyobeba majibu Yako unayoitolea Fungu la kumi lazima ijibu na ikupe mabadiliko ya Kiroho na mwili.
Ukiona huoni mabadiliko yoyote kiroho na KIMWILI Shinda Ni Madhabahu
Ukiwa Mwaminifu kwa Mungu UKAONA Upo hivyo hivyo ujue Shinda Ni Madhabahu ulipo.

HASARA

1;Hutajibiwa
2;Milango Haitafunguka
3Utaona ngumu kila unalopanga kulifanya
4:Hutaona mabadiliko yoyote
5; Madhabahu uliyonayo haitakujibu nawewe utatoa Fungu la kumi Hutaona mabadiliko kiroho na kimwili Shinda Madhabahu huitendei haki Sio Mwaminifu.

Hitimisho
Tuitimishe Kusema Mimi nimekufundisha Sijakuambia fanya hivi lakini Kupitia ufafanuzi nimejitaidi unielewe kulingana na Roho Mtakatifu anavyoongoza ndani yangu Basi Hebu fanyia kazi somo na elekeza Ufahamu wako kuona Mungu kapangilia hivyo ili wewe kukuhudumia vizuri.

Shirikisha wengine unaowapenda wajifunze kitu Kama ulichokipata wewe

Namba ya Kuungwa kwenye Group La Pastor Richard ili ujifunze mengi zaidi ukue kiroho +255759861768

🗣️onyo#
Ni kosa kuondoa au Kupunguza hata Neno Moja katika Somo Hili Kama lilivyoongozwa HUPASWI kufanya hivyo.

@2020 Pastor Richard

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NDOTO 20 ZA SHULENI TU MAZINGIRA Ya SHULE

SOMO: NGUVU YA KUJITAMBUA

SOMO:ADUI NA JINSI YA KUMKABILI ADUI YAKO.