SOMO;UTOFAUTI KATI YA MWILI ROHO NA NAFSI
SOMO; UTOFAUTI KATI YA MWILI,NAFSI, NA ROHO
Karibu Katika Darasa hili la Mafundisho Ya Neno la Mungu
Leo nataka niongelee Utofauti kati ya roho na nafsi pamoja na mwili.
Naitwa Pastor Richard
WhatsApp +255759861768
Tuanze Na
1;MWILI
Ni ngozi hii ya nje iliyofunuka na Inapokea Taarifa kutoka kwenye Nafsi.
Mwili hauwezi kufanya chochote endapo nafsi yako itakuwa inashambuliwa na adui.
●●●●
Mwanzo 6:12
[12]Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.
And God looked upon the earth, and, behold, it was corrupt; for all flesh had corrupted his way upon the earth.
2;NAFSI.
Nafsi ni uhai wa mwili kuweza kujiendesha katika hisia mbalimbali kila kiungo kuweza kufanya kazi yake vyema ni nafsi inapokuwa hai.
Mfano; hisia za Kupenda na Kuumizwa
Magonjwa au Afya Mtu ataujua mwili unauma endapo atapokea hisia za maumivu ndani yake nakupelekwa kwenye mlango husika wa kumpatia taarifa.
Nafsi ni chembechembe hai Zilizopo pale ngozi ya tatu inapochunwa.
Yaitaji ufahamu uwe vizuri kunielewa haya
Mwanzo 2:7
[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
And the LORD God formed man of the dust of the ground, and breathed into his nostrils the breath of life; and man became a living soul.
3;ROHO
Roho ni Pumzi inayokufanya nafsi yako iwe hai mwili uwe hai na Uishi.
Kazi ya Roho nikupulizia Pumzi Mwili uweze kuishi na Kufanya kazi zake kama mwili.
Roho nikiungo kilichobemba maisha yako Tunaweza kusema Kuna mtu anayeonekana kimwili lakini yupo mwingine aliyeuvaa mwili huu nakuuendesha atakavyo yeye. ROHO INAFANANA NA UNAVYOJIONA NDIYO KIUNGO KITAKACHOTOA HESABU YA MEMA YAKO NA MABAYA YAKO SIKU IKIFA GAMBA LA NJE UTALIACHA LITAZIKWA DUNIANI.
Mwanzo 2:7
[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
And the LORD God formed man of the dust of the ground, and breathed into his nostrils the breath of life; and man became a living soul.
HITIMISHO
TOFAUTISHA KAZI ZA NAFSI ROHO NA MWILI ILI UWEZE KUJIONGOZA MWENYEWE KIROHO NAKUZISHINDA TAMAA ZA MWILI.
WITO
Tumia namba hizi mfate Pastor Richard WhatsApp +255759861768 atakupa maelekezo uende Ukachukue majibu Yako yeye Anafundisha Neno la Mungu haombei.
Maoni
Chapisha Maoni