Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2026

SOMO:USHINDI WA PASAKA

Somo: Ushindi Wa Pasaka: Kutoka Gizani Kwenda Nuruni Ninayekukaribisha Somo hili Ninaitwa Pastor Richard Wa Morogoro Nataka Tukumbushane Umuhimu Wa Sikukuu ya Pasaka ​ Lengo la Somo: Kuelewa maana halisi ya kifo na ufufuo wa Yesu Kristo na jinsi unavyompa mwamini mamlaka na matumaini mapya. Nimeligawanya Somo hili Mara Tatu Ili Kukufanya Uelewe  Vizuri 1Alhamis Kuu:- Hii hutukumbusha kuwa wanyenyekevu na Wenye upendo 2:Ijumaa Kuu:- Hii Hutukumbusha Gharama ya Ukombozi Yesu Alivyokufa Kwa Ajili yetu ili tuwe na ukombozi.  3:Jumapili Ya Pasaka:- Nguvu ya Ushindi wa Vizuizi vyote na vipigamizi Vyote.  ​1. Maandalizi na Unyenyekevu (Alhamisi Kuu) ​Kabla ya ushindi, kuna utii. Yesu alituonyesha kielelezo cha upendo na utumishi kwa kunawa miguu wanafunzi wake na kuanzisha Meza ya Bwana. ​ Mstari wa Kusoma:   Yohana 13:14-15  — "Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewanawa miguu, imewapasa vivyo hivyo kunawana miguu ninyi kwa ninyi." ​2. Gharama ya Ukombozi (Ij...