Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2025

SOMO: MEZA YA BWANA

Picha
SOMO;MEZA YA BWANA. Katika biblia kuna vifungu vinne vya maandiko matakatifu vinavyoelezea vyema kuhusu meza ya Bwana. Vifungu hivyo ni; Mathayo 26:26-29 Marko 14:22-25 Luka 22:15-20 1 Wakorintho 11:23-25 Katika mafungu hayo ya maandiko tunaweza kujifunza mambo mengi,ikiwemo maana halisi ya  “meza ya Bwana  ” ,umuhimu wa meza ya Bwana katika maisha yetu ya sasa, lakini pia damu ya Yesu na umuhimu wake.  Nini maana ya meza ya Bwana? Neno“ Meza ya Bwana ” huitwa pia “ chakula cha Bwana,Karamu ya Bwana, sherehe ya Bwana ” ni Ibada maalumu ya kula mwili na damu ya Yesu ya agano. Ukumbuke,ya kwamba kuna maagizo mawili aliyoagiza Yesu yafanyike mara kwa mara ndani ya kanisa ( agizo la kwanza ni ubatizo na pili ni kushiriki meza ya Bwana Kwa ukumbusho wake). Katika meza ya Bwana kuna vitu viwili; Mkate – kumwakilisha mwili wa Yesu Divai/kikombe cha baraka au kikombe cha zao la mzabibu – huwakilisha damu ya Yesu ya agano jipya Hivyo,meza ya Bwana inaandaliwa na kuhani wa Mungu Al...

DALILI 10 ZINAZOKUJULISHA UMEITWA NA MUNGU UKAMTUMIKIE UKAOKOE ROHO ZA WATU

SOMO: DALILI 10 ZINAZOKUJULISHA UMEITWA NA MUNGU UKAWE MTUMISHI WA WATU WAKE.  Rejea Yona:1 Sura yote. Yeremia:1 Sura yote. Kutoka:3 Sura yote. Isaya. 6 Sura yote.  Watu wengi Leo Wanapitia Matatizo kwa Sababu Waliitwa wakafanye kazi ya MUNGU wakaenda kufanya vitu vingine Sasha kila wafanyacho hakiendi Audi Ameruhusiwa awatese nakuwashinda Sababu Wamekimbia Wito. Naitwa Askofu Richard Julius Kushoka Nipo Morogoro Makao Makuu ya Makanisa Ya Holy Spirit Church Tanzania.  1:Kuwa na Visingizio Visivyoisha Kwenye Wito wake. Yaani Unapopewa ratiba ya kufanya huduma kanisani una Sababu kibao kila siku Udhuru. 2:Kufatwa na Watu wengi Wanakuambia Neno lile like La Wito wa Kumtumikia MUNGU.  3:Kuota Ndoto Unahubiri au upo kanisani Ndoto za kanisani Kanisani tu mara unaombea watu unawafungua watu unawaombea.  4:Kila Kitu Kinaanza Kufa Chochote Unachofanya Kinakufa yaani unaanza kupitia majanga Yasiyoisha Yaani unajikuta unateseka KWELI KWELI.  5:Malengo Yako Yanakufa ...