SOMO;TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA
SOMO: TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA WENU. #UTANGULIZI Karibu katika nakala hii inayoenda kukupa mwanga katika kuendesha uchumba hasa kwa vijana wetu ambao wapo kwenye uchumba Mahusiano mengi yanavunjika na kutokufikia malengo kwa sababu ya ukosefu wa elimu Nayekukaribisha katika darasa hili Naitwa Mwalimu Wa Wanandoa Bishop Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa WhatsApp +255759861768 #UTARATIBU MAANA YAKE NINI Makusundi au mpangilio mzuri wa kulifanya jambo liwe katika ubora wakuonekana vyema. KUNA TARATIBU 10 ZA KUFATWA UNAPOENDESHA UCHUMBA WAKO KIBIBLIA. 1:MRUHUSUNI MUNGU AJENGE UCHUMBA WENU NA SIYO AKILI ZENU Utasoma Zaburi;127;1 Uchumba wenu mnapaswa uwe Pembe tatu Juu muwekeni Mungu kulia akae mchumba wako na Kushoto ukae wewe kama ulivyo umbali wa Pembe Tatu kutoka Pembe moja kwenda Pembe nyigine ndivyo mnavyotakiwa muishi msikaribiane. Uchumba mkiujenga nyinyi wawili Mungu mkamuweka Pembe...