SOMO;TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA
SOMO: TARATIBU 10 ZA KUENDESHA UCHUMBA WENU.
#UTANGULIZI
Karibu katika nakala hii inayoenda kukupa mwanga katika kuendesha uchumba hasa kwa vijana wetu ambao wapo kwenye uchumba Mahusiano mengi yanavunjika na kutokufikia malengo kwa sababu ya ukosefu wa elimu Nayekukaribisha katika darasa hili Naitwa Mwalimu Wa Wanandoa Bishop Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
WhatsApp +255759861768
#UTARATIBU MAANA YAKE NINI Makusundi au mpangilio mzuri wa kulifanya jambo liwe katika ubora wakuonekana vyema.
KUNA TARATIBU 10 ZA KUFATWA UNAPOENDESHA UCHUMBA WAKO KIBIBLIA.
1:MRUHUSUNI MUNGU AJENGE UCHUMBA WENU NA SIYO AKILI ZENU
Utasoma Zaburi;127;1
Uchumba wenu mnapaswa uwe Pembe tatu Juu muwekeni Mungu kulia akae mchumba wako na Kushoto ukae wewe kama ulivyo umbali wa Pembe Tatu kutoka Pembe moja kwenda Pembe nyigine ndivyo mnavyotakiwa muishi msikaribiane.
Uchumba mkiujenga nyinyi wawili Mungu mkamuweka Pembeni lazima mtakaribiana Nakuanza Kuzini Kwa Sababu kila mmoja wenu atakuwa hana hofu na dhambi.
2:WEKENI WAZI NA KURASIMISHA UCHUMBA WENU KWA WAZAZI.
Utasoma Mwanzo;4;9
Uchumba wenu usiwe wa uchochoroni au ngizani hamtaki nuru Hakikisheni Mnaenda kwa Wazazi Kujitambulisha na Hamtakiwi mkae muda mrefu mpo Kwenye uchumba usiojulikana kwa wazazi.
Hapa naongezea kwa mabint wanaopenda kujirahisha na kwenda kukaa na wanaume ambao hawajawatolea mahari sijui ni biblia ngani walipata inayowaruhusu Kujiowa. Ni vyema Bint uwe na uvumilivu na ujitambue wewe ni wathamani usianze kuzini na mtu ambaye hajakutolea mahari. Nawewe kijana wa kiume usiowe Bint anayekimbilia kuzini nawewe na siyo ndoa au anayekimbilia kukuzalia mtoto wakati hujamuowa mwepuke Bint wa Hivi.
3;JICHANGANYENI NA WATU MSIPENDE KUJITENGA KILA MNAPOONEKANA.
Utasoma mwanzo; 24;19-21
Hapa namanisha wachumba hamtakiwi mjitenge na shughuli za jamii au kuonekana kila saa mnatembea nakukaa mkiwa wawili hamtaki kujichaganya muwe watu mnaokaa na kuongea na kila mtu hata inapotokea kazi ya kikundi mfanye hivyo .
Huwa inaleta maswali mengi katika Jamii endapo mtaonekana kila saa mumejitenga nyinyi wawili iwe ni kazi za kijamii mnataka mkae au mpagwe wawili tu. Itaondoa ushuhuda mzuri ni vyema mkajichaganya.
4:LINDENI USHUHUDA WENU
Utasoma Mithali 22:1
Wachumba mnatakiwa kukumbuka mnaheshimika katika jamiii inayowazunguka na pia Mnaye Mungu Ambaye Kupitia Yeye mnaitwa watoto wa Mungu.
Jiepusheni na mazingira Haya
-Kukaa ngizani wawili
-Kukaa chumba kimoja wawili
-Kukaa mazingira tatanishi
Mnapaswa mkae sehemu za wazi au kama ni ndani msikae wawili humo muwe zaidi.
Msikumbali Mungu wenu atukanwe kwa sababu ya kupoteza ushuhuda wenu kwa jamii.
5:MSIWASHANE MOTO WA MAPENZI.
Utasoma wimbo 8:7 ,2:7
Wachumba msiaze kupeana vishawishi au kuongelea mazungumzo yatakayowafanya muaguke katika tamaa za kimwili nakuzini.
Wachumba wengi wanashindwa kufikia Lengo la ndoa kwa Sababu Ya Tamaa za Kimwili hali ambayo huwafanya wachokane mapema nakuachana.
6:WEKANENI WAZI MSIFICHANE KITU
Utasoma Waefeso:4:25
Wachumba wengi huwa wanadaganyana lengo na kusundio la wao kuanzisha uchumba ni ndoa au kuchezeana
Mambo haya yaweke wazi
-Mahusiano yako ya nyuma na sababu iliyopelekea mkaachana naye ni nini.
-Tabia usizozipenda na unazozipenda mwambie ukweli
-Uvaaji usiopenda na unaoupenda
-Kama unamatatizo ya kiafya mweleze kabla ya kuingia kwenye ndoa.
-Kazi yako unayofanya umri wako nk.
Kwenye uchumba ndipo kwenye kutengeneza ndoa iliyo na furaha na Amani usikosee mwanzo.
7;MALIZENI TOFAUTI ZENU MSIMPE NAFASI ADUI AVUNJE UCHUMBA WENU
Utasoma Waefeso;4;25
Kwenye uchumba huwa kuna hatua mtapitia ya kugombana na wakati mwigine msiongee au kutumiana sms hata simu I aisha msimpe nafasi adui awaharibie malengo Yenu hebu Tumia nafasi Soma Mathayo;6;14-15 "msipowasamehe wengine na Baba yenu wa mbiguni hatawasamehe nyinyi"Pataneni na Kuendelea tena kwa Upendo mkiweza kuvumiliana kwenye uchumba basi hata ndoa yenu itakuwa ya mfano katika jamii.
8:CHANGUENI WALEZI WA UCHUMBA WENU WANANDOA WENYE HEKIMA NA BUSARA.
Utasoma Mithali;11:14
Naposema walezi maana yake hata mkigombana kwenye uchumba wenu mtawasikiliza na kubadilika mnatakiwa kwa pamoja mkae na kukubaliana watu mtakaowachangua pia wao wenyewe ndoa yao iwe ya kuingwa katika jamii
Hao walezi watawasaindia Sana Kufanya Mahusiano yenu yafikie ndoa nawashauri msiende bila walezi.
9;TUMIENI KINYWA CHENU KUJENGA UCHUMBA WENU NA SIYO KUBOMOA.
Utasoma Yohana:13:34 Wagalatia:6;2
Kuna maneno matano yanayojenga uchumba nakuufanya mpendane msichokane
1:Neno "NAKUPENDA SANA"
Unapoandika Sms au Kuongea na mwezako kwenye simu Malizia Neno nakupenda Baby Nakupenda Sana" ipo nguvu kubwa mtu akisikia neno hilo kwa mtu ampendaye.
2;Neno "SAMAHANI SANA"
Unapojiona umemkwanza mweza wako mwambie Naomba Unisamehe Sana Nimekosa mpenzi wangu ongea naye kwa upole.
3;Neno "ANSATE SANA"
Unapopewa au kufanyiwa jambo na mwezi wako hata kama ni kidogo shukuru mwambie Ansate Sana Mpenzi Wangu.
4:Neno "UVUMILIVU WA VIPINDI"
Onesha Uvumilivu hasa mnapokuja kupita katika changamoto mbalimbali au mmoja wenu akapitia kukosa kazi mvumilie na kumuombea.
5: Neno "KUJALIANA"
Anapoumwa au Kulazwa wewe onesha unakuwa wa kwanza kumjali fatilia maendeleo yake kwa kumtumia hata sms kumpigia Simi kujua anaendeleaje Amekula Kanisani Ameenda au kuomba mkumbushe kuombea Mahusiano Yenu.
Haya ni maneno yatumie kujenga uchumba wenu
10;ANZISHA UCHUMBA UKIWA TAYARI KUOLEWA/KUOWA.
Utasoma Mithali:3;1
Usianzishe uchumba imladi uonekane tu nawewe unamtu kumbe mnapotezeana muda Tafadhali Anzisha uchumba ukiwa na Lengo LA Kuowa au Kuolewa.
Usiazishe Uchumba ukiwa na Lengo La Kuzini au mkae bila kutambulika popote
Nyinyi wawili ndiyo mtakaotuletea ushuhuda mzuri au mbaya kuheshimisha wazazi wenu au kutukanwa wazazi wenu
Unapofata taratibu au kuowa/kuolewa kwa utaratibu unaleta Heshima kwa Mungu na wazazi wako.
HITIMISHO
Mpaka hapo nimefikia mwisho wa nakala hii nakuombea ufike kanisani Morogoro veta Dakawa ili ufunguliwe kupitia masomo watu wameshaanza kuja kutoka nchi mbalimbali
WhatsApp hii utapewa maelekezo ya kufika +255759861768
Wito
Penda kujifunza zaidi na siyo kuombewa mafundisho yanakufungua ufahamu wako
Maoni
Chapisha Maoni